UFUPISHO WA KITABU THINK AND GROW RICH, SURA YA 15(MIZIMU 6 YA WOGA) | JIFUNZE UJASIRIAMALI

UFUPISHO WA KITABU THINK AND GROW RICH, SURA YA 15(MIZIMU 6 YA WOGA)

SURA YA KUMI NA TANO.
JINSI YA KUONDOKANA NA MIZIMU SITA YA HOFU.
Hebu jichunguze  mwenyewe kwanza wakati ukisoma hii sura ya mwisho kujua ni mizimu wangapi waliosimama mbele yako. Kabla hujaanza kuzitumia kanuni husika kwa mafanikio, akili yako ni lazima kwanza iwe tayari kuzipokea. Maandalizi siyo magumu, huanza na  kujifunza, kutathmini na kuwatambua maadui watatu ambao unapaswa kuwaondoa kwanza. Maadui  hao ni
1) Kusitasita.
2) Wasiwasi na
3) Hofu/Woga
Mlango fahamu wa sita kamwe hautafanya kazi kabla maadui hawa hawajaondolewa, na maadui hawa waovu hawaachani, popote pale mmoja alilpo basi ujue na  wengine wawili  hawapo mbali. Sura  hii, inaelezea hali ambayo ni lazima  mtu uifikie kabla ya kuanza kutumia kanuni hizi  13 kwa ujumla.

Kuna Hofu aina sita ambazo binadamu ni lazima akumbane nazo angalao moja au zote katika maisha yake yote.
1) Hofu ya kuwa  masikini.
2) Hofu ya kulaumiwa.
3) Hofu ya magonjwa.
4) Hofu ya kufiwa.
5) Hofu ya kuzeeka.
6) Hofu ya kufa.

Hofu huzaa  kusitasita na kumbuka  haya unaposoma. Kusitasita hujigeuza kuwa mashaka na vyote viwili huungana na kutengeneza Hofu. Mchakato huo hufanyika taratibu, na hii ndiyo sababu ya hawa maadui watatu kuwa hatari kiasi hicho. Huota na kukua pasipo kushitukiwa. (Ni kama virusi vya ukimwi vile)


<<<Kurudi sura ya 14 bofya hapa.<<<
....................................................................................


Na huo ndio mwisho wa Mapitio kwa ufupi ya Sura za kitabu cha, Think And Grow Rich, kitabu kilichoandikwa na mwandishi mashuhuri kabisa katika karne ya 20, Napoleon Hill miaka zaidi ya 70 iliyopita lakini umuhimu wake kuendelea kubakia vilevile kama ulivyokuwa na utaendelea kubakia hivyo hivyo pengine kwa vizazi vingine vingi vijavyo.

Ukipenda kusoma Kitabu chenyewe(Full) Think and Grow Rich katika lugha ya kiswahili fasaha bila chenga bonyeza maandishi yafuatayo; 



Kudownload kitabu kizima Think and Grow Rich katika lugha ya kiingereza bonyeza maandishi haya hapa chini;

0 Response to "UFUPISHO WA KITABU THINK AND GROW RICH, SURA YA 15(MIZIMU 6 YA WOGA)"

Post a Comment