MTANGAZANIA BILIONEA DONALD TRUMP WA CHAMA CHA REPUBLICAN AZOMEWA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

MTANGAZANIA BILIONEA DONALD TRUMP WA CHAMA CHA REPUBLICAN AZOMEWA

Donald Trump, Bilionea maarufu  anayemiliki majumba  nchini Marekani, ameendelea kutawala mdahalo wa kwanza katika kinyanganyiro cha kumpata mgombea urais wa Marekani kupitia tiketi ya chama cha Republican licha ya kuzomewa na wanaompinga kutokana na misimamo yake hasa juu ya sera zake za nje kama vile suala la wahamiaji kutokaMexico wanaoingia  nchini humo nakusababisha tatizo la kuongezeka magenge ya wauzaji madawa ya kulevya.

Aliwaita wanasiasa kuwa ni “wapumbavu” na kwamba alikuwa anajiandaa kuachana na chama cha Republicana na kwenda kuanzisha cha kwake. Aliwalaumu wanasiasa wa marekani kuwa ni wajinga kwa kukubali kuwapokea wahamiaji wa Kimexico wakati viongozi wa Mexico wenyewe wakionekana kuwa ni werevu na wajanja kwani huwatuma ‘wahalifu’ na ‘wabakaji’ kwenda nchini Marekani.

Watangaza nia walikuwa 17 katika mdahalo huo lakini Donald Trump ndiye aliyengara zaidi akifuatiwa na wengine wachache kama vile, gavana wa zamani wa Florida na mdogo wake Rais wa zamani George W Bush  Jeb Bush,  wengine ni Seneta wa Florida, Marco Rubio, Gavana wa Wisconsin Scott Walker na wengineo.

Atakayeibuka kidedea katika kinyanganyiro hicho atakabiliana na mgombea atakayekuwa  amesimamishwa na chama hasimu cha Democrat katika kumtafuta Raisi na kwa kiasi kikubwa imeshatabiriwa na wengi kuwa huenda akawa Bi Hillary Clinton, mwanamke wa kwanza kuwania nafasi hiyo ya juu kabisa katika Taifa hilo kubwa Duniani.



0 Response to "MTANGAZANIA BILIONEA DONALD TRUMP WA CHAMA CHA REPUBLICAN AZOMEWA"

Post a Comment