MTOTO MIAKA 8 ASAFIRISHWA KWA BEGI KAMA NGUO! | JIFUNZE UJASIRIAMALI

MTOTO MIAKA 8 ASAFIRISHWA KWA BEGI KAMA NGUO!

Mtoto mwenye umri wa miaka 8 amesafirishwa akiwa ndani ya begi mithili ya nguo akitokea nchini Morroco hadi nchini Hispania kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mofisa wa polisi nchini Hispania.


Mtoto huyo wa kiume kwa jina, Abou alikutwa ndani ya begi hilo lililokuwa limebebwa na msichana wa miaka 19 akielekea Cueta,eneo lililo karibu na nchi ya Morocco siku ya Alhamisi.


Polisi walipofungua begi hilo, mtoto huyo alikuwa katika hali mbaya sana.

Mvulana huyo kutoka Ivory Coast sasa anapewa uangalizi na mamlaka za Cueta.

Mtotot huyo akiwa ndani ya Begi

Gazeti la Uhispania El Paris liliripoti kuwa msichana huyo wa miaka 19 hana uhusiano wowote na mtoto huyo na kwamba alilipwa na baba yake mzazi ili abebe begi hilo.

Baba yake na mtoto huyo anaishi visiwani Conary na alitarajia kuonana na mwanaye kulingana na gazeti hilo.

Chombo cha habari cha Uhispania Efe kidai kwamba baba yake mtoto huyo anayejulikana kwa jina la Abou alisafiri hadi nchini Ivory Coast kumchukua mwanaye baada ya kuhamia katika eneo la Gran Canaria mwaka 2013.


Babake baadaye aliripotiwa kumlipa raia huyo wa Morocco ambaye alimsafirishia mtoto huyo akitumia begi.

Msemaji wa polisi aliiambia Efe  kuwa alionekana kusita na kama ambaye hakutaka kupitia mpakani.

                    Chanzo cha habari hii ni BBC

0 Response to "MTOTO MIAKA 8 ASAFIRISHWA KWA BEGI KAMA NGUO!"

Post a Comment