BILIONEA BAKHRESA AZINDUA RASMI AZAM TV | JIFUNZE UJASIRIAMALI

BILIONEA BAKHRESA AZINDUA RASMI AZAM TV

Siku za nyuma kulikuwa na minongono miongoni mwa jamii kuwa Bilionea Said Salim Bakhresa huwa hapendi kujionyesha hadharani, hata picha yake ni watu wachache mno waliokuwa wakiifahamu.

Mfano mzuri ni jana wakati Rais Jakaya Mrisho Kikwete alipokuwa akizindua rasmi  Azam TV jijini Dar es salaam, nilikuta vijana fulani mahali wakiitana, mmoja akiwaambia wenzake, “njooni haraka mumuone Baresa, kwenye tv, mlisema huwa haonekani sasa huyu ni nani?
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokewa na Bw. Saidi Salim Bakhressa wakati alipohudhuria sherehe za uzinduzi rasmi wa studio mpya za stesheni hiyo iliyopo Tabata Relini jijini Dar es salaam leo Machi 6, 2015.
Kumbe vijana wale kuna siku walibishana nusu wapigane, kisa eti wengine wakisema Baresa anaonekana hadharani na wengine wakibisha kabisa na kusema, Baresa hawezi kabisa kuonekana hadharani. Ni watu wengi waliokuwa wakimsikia Bakhresa kwa jina tu huku wakitamani japo siku moja waione sura yake.

Nilithibitisha hilo baada ya siku moja nilipokuwa nimeshika kitabu cha MIFEREJI 7 YA PESA NA SIRI MATAJIRI WASIYOPENDA KUITOA ambacho juu ya jalada kuna picha za Mabilionea wetu watatu,kushoto, Mzee Reginald Mengi, katikati Mzee Said Salim Bakhresa na kulia MO au Mohamed Dewj, kila aliyekuwa akikiangalia kile kitabu aliniuliza huyu hapa katikati ni nani? Ni wachache waliokuwa wakigundua kuwa ndiye Bakhresa.
Kitabu “Mifereji 7 ya pesa na siri matajiri wasiyopenda kuitoa”

Habari za uzinduzi wa Azam TV kwa kina unaweza ukazipata zaidi katika blogu hii hapa ya Tanzania Today

0 Response to "BILIONEA BAKHRESA AZINDUA RASMI AZAM TV"

Post a Comment