UWEZO WETU WA KUFIKIRI WATANZANIA NI MDOGO:TAFITI | JIFUNZE UJASIRIAMALI

UWEZO WETU WA KUFIKIRI WATANZANIA NI MDOGO:TAFITI

Bendera ya Tanzania
Tafiti za hivi karibuni na za kuaminika kutoka kwa wataalamu zinaonyesha kwamba nchi ya  Tanzania  ipo ndani ya kumi bora kutokea mkiani katika suala zima la kufikiri. Kwa kweli hili ni kama tusi kwa Watanzania  lakini linaweza likawa na ukweli kama hatuna vigezo vya maana vya kulipinga.
Ukweli huu unadhihirishwa na vigezo vingi hata mtu unapopima kwa akili ya kawaida tu. Kila siku utasikia mambo ya ajabu na ya kusikitisha yakitendeka, na mfano mzuri ni imani potofu zinaopelekea mauaji ya watu wasiokuwa na hatia kama vikongwe, wenyeulemavu, na hata watoto wadogo.

Kiashiria kingine cha utovu wa kufikiri kwa Watanzania kinadhihirika katika mambo kama vile, upinzani mkali kwa wale watu wanaojaribu kuibua masuluhisho kwa matatizo mbalimbali hususani umasikini na magonjwa. Mfano mzuri tunauona kwa Askofu Sylvester Gamanywa na kampeni yake ya kuwamilikisha vijana uchumi.

Wamediriki kujitokeza watu tena wenye dhima kubwa tu katika jamii waliodiriki kuonyesha upinzani wa ajabu kwa kudai eti yeye Gamanywa ameingiza biashara kanisani, tena biashara za ‘Kishirikina”, wamemhusisha na vyama/taasisi zisizoeleweka. Huo ni uvivu mkubwa wa kufikiri, mtu kujaribu kumsingizia mwenzake mambo yasiyoeleweka ilihali mtu huyo anachofanya ni jambo la kheri lenye lengo la kuwakomboa watu kutokana na umasikini.

Inawezekana pia kuwa ni wivu tu, mtu anaona anachofanya mwenzake ni kitu kizuri, sasa ili na yeye aonekane au kusikika, basi anajaribu kuponda. Gamanywa inafaa apewe moyo, na siyo yeye tu, mtu yeyote anayejaribu kuleta suluhisho la kweli la umasikini haipaswi tumkatishe tamaa, haijalishi ni wa dini gani, awe mkristo awe Muislamu, awe Mhindi, tusiangalie dini wala kabila bali tuangalie tutaondokaje pale tulipo.

Watanzania tuache imani potofu za aina yeyote ile zinazolenga kuturudisha nyuma kimaendeleo, suluhisho la matatizo yetu mengi ni kuutokomeza umasikini na umasikini hauwezi ukaondolewa kwa ushirikina, hila wala imani potofu, bali ni kwa kufanya kazi kwa bidii huku tukifuata kanuni bora za kisayansi zilizothibitika  na zilizoweza hata kuwatoa na kuwakomboa  Wamarekani, Wachina, na Mataifa yote yaliyopiga hatua kimaendeleo.

Hebu sikiliza kidogo audio hizi zinazohusu BCIC na kampeni nzima ya Askofu Sylvester Gamanywa juu ya kuwarithisha vijana ili waweze kuondokana na umasikini wa kipato.




0 Response to "UWEZO WETU WA KUFIKIRI WATANZANIA NI MDOGO:TAFITI"

Post a Comment