PAKA SHUJAA: AMUOKOA MTOTO ALIYETAKA KUUMWA NA MBWA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

PAKA SHUJAA: AMUOKOA MTOTO ALIYETAKA KUUMWA NA MBWA




Ni tukio la ajabu na ni la nadra sana kutokea. Paka mmoja amemuokoa rafiki yake mtoto mdogo wa kiume wakati mtoto huyo alipokuwa akishambuliwa na kuburutwa na Jibwa la jirani yao linalosadikiwa kuwa na kichaa cha mbwa.

Mtoto huyo mkazi wa Kusini Magharibi mwa Bakersfield California kwa jina Jeremia, miaka 4 ambaye inasemekana ana ulemavu kidogo wa akili (mtindio wa ubongo lakini kwa kiasi kidogo)  siku ya Jumanne wiki hii alipokuwa akitoka shuleni na baiskeli yake kuelekea nyumbani, alisimama kidogo akirusha kishada chake ndipo nyuma yake ghafla likaibuka jibwa (mbwa) la jirani yao na kuanza kumng’ata huku likimburura.

Mtoto Jeremy Triantafilo akiwa na shujaa wake paka aliyemuokoa.

Paka wa nyumbani kwa Jeremia aitwaye ‘Tara’ naye kumbe hakuwa mbali na pale, alitokea ghafla na kwa sekunde chache  akamkimbilia na kumrukia yule mbwa huku akimkimbiza. Tukio hili la aina yake liliweza kurekodiwa  live na kamera za usalama za cctv

“Tara ni shujaa wangu”  Alisema Jeremia

Mama wa mtoto huyu aitwaye Erika Triavitafilv naye alikuwa karibu na eneo lile la tukio akimwagilia maji maua ndipo akasikia mtoto akipiga mayowe ya kuomba msaada. Mama huyo hakuamini kile lilichokuwa kimetokea mpaka pale mumewe alipokuja kumuonyesha ile video hiyo ya usalama.

Anasema mtoto hakuumia sana, na alipewa matibabu hospitalini, huku hali yake ikiendelea kuimarika. “Sijawahi kumuona Paka akifanya kitendo cha namna ile”  alisema baba wa mtoto Jeremy


Polisi walisema mbwa aliyehusika kwa sasa yupo chini ya uangalizi maalumu na wataendelea kumuangalia kwa kipindi cha siku kumi kisha watamuua kwa sindano ya sumu.

0 Response to "PAKA SHUJAA: AMUOKOA MTOTO ALIYETAKA KUUMWA NA MBWA"

Post a Comment