MUZIKI MPYA MKALI 'KITORONDO' WA DIAMOND NI GUMZO LA JIJI: UDOWNLOAD HAPA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

MUZIKI MPYA MKALI 'KITORONDO' WA DIAMOND NI GUMZO LA JIJI: UDOWNLOAD HAPA

Diamond Platnumz .



….Nimetembea tembea Bara na visiwani, ila nikajionea….Natamani nikupe ..hela sinaaa…Nimejaliwa pendo, heshimaa ….Wana wivu hao, haoo… hao,  wachonganishi hao,  haoo hao….Usijeniacha kwa unyonge, nitachechemea ….
……Mwendawazimu kaingiaje… Kitomondo kitomondo… mwendawazimu kaingiaje……
,,,,,,,KITOMOMDO…….KITOMONDO……
…WANA WIVU HAO..HAOOO… HAO….

Hivyo ni baadhi tu ya vionjo vilivyopo ndani ya mashairi ‘lyrics’ ya  ‘songi’ hili kali “KITOMONDO” la mkali Diamond Platnumz linalotarajiwa kutoka rasmi hivi karibuni, kwani hii ‘version’ siyo halisi hata ukisikiliza tu sauti yake (ubora) siyo wenyewe original, ni wajanja tu kama ujuavyo Bongo yetu, wameamua kuvujisha kitu kabla hata mwenyewe Diamond hajakiweka hadharani ‘oficially’.

Kwa kweli siyo jambo zuri kabisa hata kidogo, hali hii inarudisha sana nyuma maendeleo ya muziki na wajasiriamali wanaotaka kutoka kupitia fani hii. Ingefaa sana serikali kupitia sheria zake ikakaza zaidi ile sheria ya haki miliki ya kazi za ubunifu na sanaa ili hapo baadaye kuondoa kabisa ujanja ujanja huu ambao katika nchi za wenzetu hata kama upo siyo kwa kiasi cha kutisha kama ilivyokuwa hapa kwetu Tanzania.

0 Response to "MUZIKI MPYA MKALI 'KITORONDO' WA DIAMOND NI GUMZO LA JIJI: UDOWNLOAD HAPA"

Post a Comment