JEFRYDER NDANI YA EAST AFRICA TV NA VIDEO YAKE NIPE MIC | JIFUNZE UJASIRIAMALI

JEFRYDER NDANI YA EAST AFRICA TV NA VIDEO YAKE NIPE MIC




Yule Msanii wa Hip hop anayechipukia na ambaye tayari ameshaachia ngoma kali mbili, Nipe love na Nipe Mic Jafary Ahmed au kwa jina la usanii Jefryder, Jana alifanya mahojiano na kipindi cha Luninga EATV cha Five Select kinachoruka hewani kila siku ya Jumanne saa 9 alasiri. Katika show hiyo Jefryder alikuwa akiitambulisha video ya wimbo wake wa NIPE MIC ambapo baada ya kuulizwa kwa nini kila kitu kibaya lazima kiwe Hip Hop, “hazihitaji kuonyesha mbwembwe nyingi kwenye jengo bovu nini”

Alijibu kuwa hivyo ndivyo nature ya hip hop ilivyo, pia alielezea kwamba wakati ‘akiishoot’ ngoma hiyo kuna msanii mmoja muhimu na aliyemtegemea ‘alimzingua’ lakini siyo kwa makusudi bali alikuwa ametingwa na shughuli nyingine za kimuziki hivyo ilimbidi Jefryder kumuomba mshkaji mwingine kuokoa jahazi na mambo yakaenda kama yalivyokuwa yamepangwa.

Tunaomba radhi kwa ubora wa hali ya chini (poor quality) katika video  inayomuonyesha msanii huyo wakati akiwa EATV. 

0 Response to "JEFRYDER NDANI YA EAST AFRICA TV NA VIDEO YAKE NIPE MIC"

Post a Comment