JE, UNAMILIKI BLOGU NA HUJAGUNDUA MABADILIKO GOOGLE WALIYOFANYA KUWEKA KURASA: PAGES? | JIFUNZE UJASIRIAMALI

JE, UNAMILIKI BLOGU NA HUJAGUNDUA MABADILIKO GOOGLE WALIYOFANYA KUWEKA KURASA: PAGES?


Ilinitokea kama bahati mbaya, nikiwa katika harakati zangu za kupanga kurasa(pages)  pale juu kwenye hii blogu chini ya ‘header’, “nikajikuta “nimedelete”  nimefuta ‘page’ ukurasa wangu wa ‘MICHANGANUO’ niligadhabika sana, ikanibidi  nianze kazi nisiyokuwa nimeitarajia ya kutengeneza tena ukurasa mwingine mpya pamoja na kujaza ‘contents’.

Mshangao mwingine tena ulinikuta baada ya kila nilipojaribu kubofya mahali palipoandikwa ‘New page’ ili nitengeneze ukurasa mwingine, inakuja ‘wizard’  tofauti kabisa na ile ya zamani tuliyoizoea, inakuruhusu kutengeneza ukurasa lakini ukurasa huo ni ule  ‘static’ peke yake, yaani mfano kama unaotumika kuweka ‘contacts’ au makala ambayo unataka isiwe inabadilika na kusogea pale ulipoiweka, mfano ni huo ukurasa wangu wa michanganuo. Walivyofanya ni sasa hivi, ukitaka kutengeneza page static hamna tofauti na kama vile unavyotengeneza ‘new post’ ya kawaida.

 Zamani ‘wizard’ hiyo ilikuruhusu kutengeneza aina zote mbili za kurasa mahali pamoja na kukuruhusu uzipange palepale kama uziweke pale juu karibu na ‘header’ zilale, zionekane kama 'static websites’ ama uzipange pembeni. zisimame wima.


Wakati nashangaa, nilidhania labda ‘Template’ yangu ‘imecrush’ na kupoteza baadhi ya ‘codes’, nikaanza kufikiria uwezekano wa kubadili nyingine, ambapo ingenichukua tena muda mwingi kwenda ‘kudownload’  na mambo mengine chungu nzima. Lakini sikukubali, nikaanza kazi ya kutafiti ‘google’, na katika pita pita yangu baada ya kuhangaika sana kubonyeza hapa na pale, nikakutana na maandishi; The latest from Blogger Buzz, Making it easier to manage pages on your blog” mwanzoni kabisa kwenye ‘dashboard’.

Haya maelezo niliwahi kuyaona kabla zaidi ya wiki moja nyuma lakini kutokana na kutozingatia sikujishughulisha kuyasoma. Lakini cha ajabu Google bwana sijui wakoje, maelezo yao pale yanaeleza kabisa wamebadilisha namna ya kupanga pages, lakini sasa ni jinsi gani tena, hakuna maelezo ya kutosha kwa mtu wa kawaida kama mimi.

Mwishoni nikaja kubaini kupitia utundu wangu kumbe ili uweze kufanya ‘arrangement’ ya ‘pages’ zako kama zamani ikiwa ni pamoja na kuunda ‘dynamic pages’ inakubidi uende mpaka kwenye ‘Layout page gadget’ kama vile unataka kuweka ‘image’, ‘html’ au ‘javascript’ isiyobadilika mfano kwenye header au katika 'sidebar'. wameongeza hiyo ‘gadget’  pale kwa ajili ya kuongeza kurasa ‘pages’. Tatizo lingine nililoliona katika mfumo huu mpya ni kwamba zile 'dynamic pages' huwezi tena 'kuziedit' moja kwa moja, ni mpaka uifute na kisha kama ni masahihisho basi utengeneze mpya.

Kwa kweli ‘it’s a really comfusing task’  hasa kwa mtu wa kawaida asiyekuwa na uzoefu sana na maswala haya ya kublog ingawa wao wamedai wanataka kurahsisha zaidi kama wanavyosema hapa  chini’

 “To make managing pages easier, we redesigned the ‘Pages’ tab in the Blogger dashboard to make it look and feel more like something you’re already familiar with: managing posts.




0 Response to "JE, UNAMILIKI BLOGU NA HUJAGUNDUA MABADILIKO GOOGLE WALIYOFANYA KUWEKA KURASA: PAGES?"

Post a Comment