JUMA NATURE AKANUSHA 'KUMDISI' DIAMOND KWENYE WIMBO WAKE NA JAYD, KAMA JANA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

JUMA NATURE AKANUSHA 'KUMDISI' DIAMOND KWENYE WIMBO WAKE NA JAYD, KAMA JANA

Mkongwe wa muziki wa kizazi kipya  Sir Juma Nature, amekanusha tetesi zilizozagaa kwenye mitandao kwamba wimbo wake mpya aliomshirikisha Lady Jaydee, unaoenda kwa jina  la ‘KAMA  JANA’, kwamba amemponda Mwanamuziki mwenzake Diamond Platnumz. Akizungumza kwenye kipindi cha NEW CHAPTER kinachorushwa hewani na Radio free Afric siku ya Jumanne mchana alisema kwamba mtu aliyemlenga katika wimbo huo siyo Diamond bali ni mtu mwingine kabisa ambaye anaishi mtaani kwao anayeitwa ‘Dada mondi’.

Juma Nature
Akielezea sababu za kubadili mtindo aliokuwa akiutumia zamani alisema kwamba anataka awe tofauti, na watu wengine  na sasa hataki tena kuimba miziki ya ‘kijinga kijinga’. Alisema pia kuwa ngoma  yake ya mwisho kabla yaii mpya baada ya kipindi kirefu ilikuwa ni ile iliyoitwa Dogo na iliyofanya vizuri pia. Vile vile alisema kwamba wanamuziki waliovuma siku za nyuma wengi wamepotea na moja ya sababu ni kuwa inachangiwa na baadhi ya watu wasiopenda wasikike ila yeye anasema kinachomlinda asipotezwe kabisa ni mashabiki wake.


 Sikiliza wimbo wake huo hapa chini;

0 Response to "JUMA NATURE AKANUSHA 'KUMDISI' DIAMOND KWENYE WIMBO WAKE NA JAYD, KAMA JANA"

Post a Comment