UGONJWA ULIOMUUA MBUNGE WA CHALINZE MH. 'SAID BWANAMDOGO' | JIFUNZE UJASIRIAMALI

UGONJWA ULIOMUUA MBUNGE WA CHALINZE MH. 'SAID BWANAMDOGO'

Mh.Said Ramadhani Bwanamdogo enzi za uhai wake.
KIlichomuua Mbunge wa Chalinze Mh. Said Bwanamdogo kinajulikana kwamba ni ugonjwa uliokuwa ukimsumbua kwa muda mrefu na habari za kulazwa kwake katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha Moi zilianza kuwa hewani takriban wiki mbili zilizopita.

Hata hivyo taarifa zaidi za ni ugonjwa gani huo uliokuwa ukimsumbua bado hazijawekwa hadharani, huku Bunge chini ya Spika Mama Anna Makinda likiendelea na maandalizi ya mazishi ya Mbunge huyo aliyefariki leo asubuhi Jumatano ya  tarehe 22/1/2014 .

Awali ilikuwa imeelezwa kwamba Mbunge huyo alikuwa mahututi Moi  na taratibu za kumpeleka nje ya nchi kwa matibabu zaidi zilikuwa zikifanywa. Baadhi ya wabunge wenzake kutoka Mkoa wa Pwani akiwemo,  Dr Seif Rashid wa Rufiji na naibu waziri wa afya pamoja na Mh Koka mbunge wa Kibaha mjini walimtembelea hospitalini hapo hivi karibuni.

Poleni wananchi wote wa Jimbo la Chalinze na Watanzania kwa ujumla na Mwenyezi  Mungu ailaze Pema Peponi Roho ya Marehemu AMINA.


0 Response to "UGONJWA ULIOMUUA MBUNGE WA CHALINZE MH. 'SAID BWANAMDOGO' "

Post a Comment