UMILIONEA WA BSS 2013 WAMWANGUKIA MUUZA MITUMBA WA JIJI LA MWANZA EMANUEL MSUYA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

UMILIONEA WA BSS 2013 WAMWANGUKIA MUUZA MITUMBA WA JIJI LA MWANZA EMANUEL MSUYA



Ritta Paulsen, Mkurugenzi(MD) wa  Bench Mark Production waandaaji wa shindano la BSS, akimkumbatia Emanuel Msuya ambaye ndiye mshindi namba 1 mwaka huu wa 2013

Hayawi Hayawi hatimaye leo  hii alfajiri yamekuwa baada ya kijana  Emanuel Msuya mjasiriamali mdogo kutoka jijini , Mwanza kujishindia Tsh.Milioni 50 pesa taslimu za Kitanzania katika kinyanganyiro cha kumtafuta mshindi wa kipaji cha kuimba katika shindano la Epiq Bongo Star Search 2013 lililofanyika jana katika klabu ya Escape jijini Dar es salaam.


Aliyekamata namba 2 Elizabeth Mwakijambile akifurahi jukwaani


Watatu bora, kuanzia kushoto ni Elizabeth Mwakijambile, Emanuel Msuya na kulia ni Melisa John.


Timu ya majaji walioamua shindano hilo ikiongozwa na Madam Ritta katikati, ambaye ndiye Jaji mkuu na mkurugenzi wa Kampuni iliyo andaa mashindano hayo, kushoto ni Banana Zoro na kulia ni Joackim Kimaro au Master J.


'Nyomi’ ya Mashabiki waliofika kushuhudia shindano hilo wakishangilia kwa furaha.

Picha zote na Maganga one blog

0 Response to "UMILIONEA WA BSS 2013 WAMWANGUKIA MUUZA MITUMBA WA JIJI LA MWANZA EMANUEL MSUYA"

Post a Comment