PICHA ZA NGONO NA NUSU UCHI ZIMEPUNGUA MAGAZETINI | JIFUNZE UJASIRIAMALI

PICHA ZA NGONO NA NUSU UCHI ZIMEPUNGUA MAGAZETINI




Msichana akiwa maziwa wazi, nusu uchi
Bi Clare Short, aliyekuwa waziri wa Mambo ya nje wa Uingereza na Mbunge wa jimbo la Birmingham amesema kwamba ,vitendo vya udhalilishaji wa wanawake kupitia picha chafu za ngono na nusu uchi katika vyombo vya habari hususani magazeti sasa vimepungua kwa kiasi kikubwa kufuatia kampeni yake na wanawake kwa ujumla waliyoianzisha tangu miaka ya 80, ijapokuwa lakini ule ukurasa maarufu katika gazeti la the sun unaochapisha picha ya msichana aliye nusu uchi, kifua na maziwa vyote vikiwa nje haujapigwa marufuku.

Alikuwa akizungumza na BBC kati kati ya jiji la London yalipo makao makuu ya bbc kwenye Tamasha kubwa la wanawake 100, lililoandaliwa na bbc yenyewe kwa mwezi mzima wa oktoba kwa ajili ya kuangazia maswala mbalimbali yahusuyo kinamama na watoto wa kike kwa ujumla katika tasnia nzima ya habari.

Tangu mwaka 1986, Bibi Short amekuwa katika vita kali dhidi ya magazeti , hususan gazeti maarufu la udaku la THE SUN juu ya ukurasa maarufu uliozua gumzo kubwa ujulikanao kama “Page 3” Ukurasa wa 3 ambao hutoa picha kila toleo ya msichana kigoli aliyevaa nusu uchi, akiacha sehemu yote ya juu  uchi kuanzia kiunoni, maziwa na kifua vyote vikiwa wazi.
 
Bi Clare Short, aliyeibua kashfa ya rada

Alifikia hatua ya kuwasilisha mswada bungeni kutaka itungwe sheria ya kupiga marufuku kurasa kama hizo lakini kwa bahati mbaya juhudi zake ziligonga mwamba pale spika alipoukataa. Hata hivyo nje ya Bunge Gazeti lenyewe la The Sun liliendesha kampeni kali dhidi yake ya kumdhalilisha na kumdhihaki, kwa mfano katika ukurasa huo wa 3 waliweka picha ya Short ikimuonyesha mnene, na kisha wakaweka maandishi, “A VERY FAT PAGE 3 GIRL” Walituma waandishi nyumbani kwake wakamuwinde usiku na mchana ili kumpiga picha za kumdhalilisha hata mbele ya mama yake mzee aliyekuwa na umri zaidi ya miaka 80.

Chanzo, The Independent

0 Response to "PICHA ZA NGONO NA NUSU UCHI ZIMEPUNGUA MAGAZETINI"

Post a Comment