MASIKINI: MTOTO WA KIKE ALIYEDHOOFU AKUTWA UCHI NDANI YA BUTI LA GARI | JIFUNZE UJASIRIAMALI

MASIKINI: MTOTO WA KIKE ALIYEDHOOFU AKUTWA UCHI NDANI YA BUTI LA GARI

Buti la gari alimokutwa mtoto wa kike
Mtoto mdogo wa kike aliyedhoofu na anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 15 amekutwa ndani ya buti la gari huko nchini Ufaransa na tayari wazazi wake wote wawili wameshatiwa mbaroni na polisi huku uchunguzi ukiendelea.

Fundi gerji eneo la Terraso alisema, walisikia sauti ya mtu aliyekuwa akilia kutoka nyuma ya gari ambalo lilikuwa limeletwa pale gereji kwa ajili ya matengenezo ndipo walipomkuta mtoto mwenye umri kati ya  miaka 15 hivi akiwa uchi, na aliyechoka kwa homa akiwa amelala chini ndani ya buti la gari.
 
Nyumba wanamoishi wananDoa hao wawili na watoto wao
Mama yake hakutaka kuweka wazi umri wa mtoto, na wote wawili yeye pamoja na mumewe waliwekwa chini ya ulinzi mkali wa polisi kwa tuhuma za kumpa mateso makali mtoto. Wakati huo huo watoto wao wengine watatu walichukuliwa na kwenda kutunzwa katika kituo cha ustawi wa jamii. 

Chanzo ni BBC

0 Response to "MASIKINI: MTOTO WA KIKE ALIYEDHOOFU AKUTWA UCHI NDANI YA BUTI LA GARI "

Post a Comment