‘Wajanja' wanatorosha Dola 2 bilioni | JIFUNZE UJASIRIAMALI

‘Wajanja' wanatorosha Dola 2 bilioni


Arusha. Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali,(PAC) Zitto Kabwe amesema kiasi cha Dola 2 bilioni za Marekani, zinapotea serikalini kila mwaka kwa kutoroshwa nje ya nchi au katika ukwepaji wa kodi .
Zitto alitoa taarifa hiyo jana, wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Arusha.
Zitto, alisema hata hivyo tatizo hilo, si tu kwa Tanzania pekee yake na kwamba taarifa za kimataifa zinaeleza kuwa kwa bara la Afrika , kiasi cha Dola 700 bilioni zanatoroshwa nje ya bara kila mwaka.
Alisema fedha hizo ni zaidi ya misaada yote inayotolewa kwa nchi za Afrika.
Chanzo ni Gazeti la Mwananchi.


0 Response to "‘Wajanja' wanatorosha Dola 2 bilioni"

Post a Comment