ALIYEMLA MWENZAKE PUA MACHO SIRI YAFICHUKA. | JIFUNZE UJASIRIAMALI

ALIYEMLA MWENZAKE PUA MACHO SIRI YAFICHUKA.

Utajiri ndio uliomponza.

Gazeti la Sani limeandika kwamba yule jamaa aliyemtafuna mwenzake kama kitoweo baada ya kumnyonga mbwa na kuumeza ulimi wake imedaiwa kumbe, alipewa masharti hayo na mganga wa kienyeji. Mganga huyo alimpa na hirizi ya simba ili imsaidie kwenye biashara zake.


Matukio ya watu kulaghaiwa na waganga wa kienyeji pamoja na imani potofu za kishirikina huleta hasara na maafa makubwa kushinda hata “Uchawi wenyewe” Kutajirika na maswala ya kishirikina ni vitu viwili tofauti kabisa, ni kama mafuta na maji, na wala haviwezi vika kaa pamoja, angalia sasa huyu jamaa badala ya kupata utajiri anaenda kuozea jela!



Kutajirika kunatokana na kufanya kazi/biashara pekee huku mtu akifuata kanuni za Ujasiriamali, na kanuni hizo wala hazimhitaji mtu kuwa na kitu cha ziada sana mfano elimu kubwa, umaarufu au fedha nyingi. Moja kati ya kanuni/sifa hizo ni uvumilivu, kubana matumizi, kuwa na malengo, kutumia muda vizuri,  na nyinginezo nyingi kama zilivyofafanuliwa katika semina na vitabu vya waandishi mbalimbali nchini na hata nje ya nchi vikiwemo pia na  vitabu maarufu vya SELF HELP BOOKS PUBLISHERS LIMITED.

0 Response to "ALIYEMLA MWENZAKE PUA MACHO SIRI YAFICHUKA."

Post a Comment