MOSES KULOLA, ASKOFU MKUU E.A.G.T AFARIKI DUNIA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

MOSES KULOLA, ASKOFU MKUU E.A.G.T AFARIKI DUNIA

Askofu Mkuu wa Kanisa la E.A.G.T na mhubiri wa kimataifa wa siku nyingi, Moses Kulola amefariki dunia. Askofu Moses Kulola amefariki leo.


Mtoto wa Askofu Kulola, ambaye naye pia ni mhubiri wa kimataifa na mchungaji wa kanisa la EAGT Lumala mpya,  Mch. Daniel Moses Kulola amethibitisha taarifa hizo kupitia katika akaunti yake ya Facebook. Kwa kuandika hivi: "WATU WA MUNGU SALAAM, NINA SALAAM ZA MAJONZI. BABA YANGU MZEE KULOLA AMEFARIKI MUDA SIYO MREFU."

Hivi karibuni  marehemu alilipotiwa kulazwa katika hospitali ya Bugando iliyopo mkoani Mwanza kwa matibabu kutokana na matatizo ya kiafya yaliyokuwa yanamkabili lakini Agosti 22 mwaka huu mwanaye Mch. Daniel Moses Kulola alieleza kuwa baba yake karuhusiwa  baada ya kupata nafuu.
MUNGU AILAZE ROHO YA ASKOFU KULOLA MAHALI PEMA PEPONI. AMEN

0 Response to " MOSES KULOLA, ASKOFU MKUU E.A.G.T AFARIKI DUNIA"

Post a Comment