WATOTO WAFUNGIWA NDANI NA MIFUGO MIAKA 8 BILA KUONA NJE | JIFUNZE UJASIRIAMALI

WATOTO WAFUNGIWA NDANI NA MIFUGO MIAKA 8 BILA KUONA NJE

Ni tangu kuzaliwa
Hawajawahi kuonana na binadamu.....


Watoto watatu huko Accra nchini Ghana, wasichana wadogo wawili na watatu mkubwa, mvulana wa miaka 8 wamekuwa wakishirikiana chumba kimoja na mifugo, bata, kuku na kondoo huku wakiwa hawajawahi hata siku moja kuonana na binadamu wengine wowote zaidi ya wazazi wao tangu walipozaliwa.
Mwandishi, Beatrice Adu wa mtandao wa Joys News, aliyekuwepo katika eneo la nyumba walimokutwa watoto hao katika mji wa Madina alisema, watoto hao watatu walikuwa wakiishi katika mazingira machafu kupindukia.

Alisema sehemu ya nyuma ya  nyumba inayoelekea vyumba vinne vya kulala kulikuwa na zizi la mifugo lililojaa mabata mizinga, kuku, na kondoo. Maeneo kuzunguka nyumba yalijaa magugu, Beatrice alisema. Akaongeza kwamba na korido inayoelekea chumba cha watoto hao ilijaa harufu mbaya na uvundo mzito.

Wakizungumza na Beatrice watoto hao walimuambia kwamba, wazazi wao walikuwa wakiwaambia kwamba kila mtu nje ya nyumba yao alikuwa mbaya. Mama wa watoto hao, Jane Mensah, alisema watoto hawaendi shuleni kwasababu baba yao Fledge Mensah Lartey anaweza kuwafundisha mwenyewe nyumbani.

Kamanda wa Polisi wa Madina aliuambia mtandao wa Joy News kwamba, ofisi yake ikishirikiana na kitengo cha ustawi wa jamii walikuwa wanaandaa makazi ya muda kwa watoto hao wakati uchunguzi zaidi ukiendelea.

Naye Daktari mkuu wa magonjwa ya akili Dr.Kwasi Osei alisema wazazi wa watoto hawa hasa baba yao inawezekana wanasumbuliwa na ugonjwa wa akili, ‘uwendawazimu’  Ugonjwa ambao unamfanya mtu kuwa na hofu ya vitu visivyojulikana. “Mtu anayesumbuliwa na ugonjwa huu hufikiria watu wengine wanaomzunguka wanamuwinda yeye na watoto wake na hivyo kuwazuia wasichanganyike na watu wengine. Wanaamini watu wengine ni ‘shetani’, watu waovu.

CHANZO: Mtandao wa myjoyonline.com


0 Response to "WATOTO WAFUNGIWA NDANI NA MIFUGO MIAKA 8 BILA KUONA NJE"

Post a Comment