David Cameron, Waziri Mkuu wa Uingereza, amekiri kuwa Rais Bashar
al Assad wa Syria ameimarisha nafasi yake katika miezi ya hivi
karibuni.
Akizungumza katika mahojiano ya BBC nchini humo, Waziri Mkuu wa
Uingereza amesema, serikali ya Syria hivi sasa imepata nguvu zaidi
ikilinganishwa na ilivyokuwa miezi michache iliyopita.
David Cameron hata hivyo amesema kuwa, London bado ina dhamira ya
kuyasaidia makundi ya wanamgambo nchini Syria licha ya kutupilia mipango
yake ya kuyapa silaha makundi hayo.
Ripoti mbalimbali zinasema kuwa, Waingereza wanapinga sana nchi yao kuwatumia silaha waasi wa Syria.
Nchi za Magharibi ikiwemo Uingereza pamoja na waitifaki wao wengine
wa eneo la Mashariki ya Kati wamekuwa wakiyatumia silaha makundi ya
kigaidi yanayofanya mauaji ya watu huko Syria kwa zaidi ya miaka miwili
sasa.
0 Response to "Cameron: Serikali ya Assad ina nguvu sasa."
Post a Comment