HABARI MUHIMU SANA KUHUSU KILE KITABU MASHUHURI ZAIDI CHA THINK & GROW RICH(FIKIRI UTAJIRIKE) | JIFUNZE UJASIRIAMALI

HABARI MUHIMU SANA KUHUSU KILE KITABU MASHUHURI ZAIDI CHA THINK & GROW RICH(FIKIRI UTAJIRIKE)


Kitabu mashuhuri cha wakati wote katika tasnia ya elimu ya fedha na mafanikio, THINK AND GROW RICH kilichoandikwa na mwanamafanikio Napoleon Hill miaka zaidi ya 80 iliyopita kwa muda mrefu kimekuwa kikichapishwa hapa katika blogu hii ya jifunzeujasiriamali katika lugha ya Kiswahili kwa tafsiri ya FIKIRI UTAJIRIKE au MSAHAFU WA MAFANIKIO.

Lakini majuma machache yaliyopita tulibadilisha uamuzi huo na kuanza kutoa tafsiri hiyo ndani ya Group la WAHATSAP la masomo ya michanganuo na mzunguko wa fedha la MICHANGANUO ONLINE, group ambalo kimsingi  washiriki wake hujiunga kwa kulipia kiingilio cha shilingi elfu 10. Baada ya kuchapisha sehemu chache za kitabu hicho kwenye group hilo, wapenzi wengi wa mfululizo huo waliokuwa wakifuatilia katika blogu walituma malalamiko yao wakitaka tafsiri hiyo irudishwe kwenye blogu kiasi cha baadhi yao hata kutoa maneno makali.


Kwa kuwa sisi lengo letu kubwa halipo kwenye faida kama wapenzi hao wengi walivyodai, kuweka kiingilio au kuuza baadhi ya huduma na bidhaa kama vitabu lengo kubwa ni kuweza kuzitegemeza huduma hizi tu kwani zinahitaji gharama mbalimbali ili kuendelea kuwepo hewani. Hata hivyo uogozi na timu nzima ya jifunzeujasiriamali baada ya kutafakari kwa kina imeamua kubatilisha uamuzi wake wa kuhamishia Think & Grow Rich kwenda katika Group la Michanganuo na kurudi kwenye blogu hii kama zamani. 

Uamuzi huo umezingatia kwamba wote, wapenzi wa blogu hii waliopo katika group na hata wale walioko kwenye utaratibu wetu wa masomo kwa njia ya email, tunawathamini wote na tusingelipenda hata mmoja kujisikia anabaguliwa. Kwa kuwa wote waliopo katika group wanaweza kuingia kwenye blogu basi nao wataendelea kufuatilia tafsiri hiyo  kwenye blogu kama kawaida.

ASANTE SANA.
Peter A. Tarimo
Self Help Books Tanzania.
Simu:    0712202244
Wasap: 0765553030

0 Response to "HABARI MUHIMU SANA KUHUSU KILE KITABU MASHUHURI ZAIDI CHA THINK & GROW RICH(FIKIRI UTAJIRIKE)"

Post a Comment