PESA BILA AKILI NI HATARI, NI NYENZO KUBWA YA MAFANIKIO IKITUMIKA VIZURI | JIFUNZE UJASIRIAMALI

PESA BILA AKILI NI HATARI, NI NYENZO KUBWA YA MAFANIKIO IKITUMIKA VIZURI



Maajabu Yaliyoleta Baraka Hizi

Nikiwa sina agenda ya siri wala kinyongo cha kuelezea, na bila ya dhamira ya moyoni, nina bahati ya kuchambua kwa uwazi maajabu hayo yasiyoshikika, kitu kinachochanganya  sana ambacho hutupatia baraka hizo zilizotangulia kutajwa, fursa za kukusanya utajiri na uhuru wa kila aina.

Ninayo haki ya kuchambua chanzo na asili ya hii nguvu isiyoonekana kwasababu nafahamu na nimekuwa nikifahamu kwa zaidi ya robo karne wengi wa watu ambao walitumia nguvu hiyo na wengi ambao sasa wanahusika kuiendeleza. Jina la mfadhili huyu wa ajabu ni MTAJI. Mtaji hauhusishi pesa tu peke yake, lakini zaidi sanasana ni makundi ya watu  waliojipanga vizuri sana, ambao hupanga njia na namna ya kutumia pesa kwa ufanisi kwa manufaa ya jamii na kwa faida yao wenyewe.

Makundi hayo hujumuisha wanasayansi, waelimishaji, wafamasia, wagunduzi, wataalamu wa biashara, wataalamu wa mahusiano ya jamii, wataalamu wa usafirishaji, wahasibu, wanasheria, madaktari na wote manaume na wanawake waliokuwa na ujuzi wa kipekee sana katika nyanja zote za viwanda na biashara. 

Huongoza, kufanya majaribio, na kuweka alama katika nyanja mpya za ubunifu. Wanasaidia vyuo, mahospitali na shule, kujenga barabara nzuri, kuchapisha magazeti, kulipa nyingi ya gharama za serikali na kulinda mahitaji mengi makubwa na madogo muhimu kwa maendeleo ya binadamu.

Kwa kifupi Mabepari ndio vichwa vya ustaarabu kwa sababu ndio huweka mfumo mzima uliobeba elimu yote, mwangaza na maendeleo ya binadamu. Pesa bila akili mara zote ni hatari. Ikiwa zitatumika vizuri, ni nyenzo muhimu zaidi ya ustaarabu.

Kifungua kinywa rahisi kwa familia katika jiji huwa na juisi ya chungwa, nafaka, mayai, mkate na siagi na chai yenye sukari. Kisingeliweza kutolewa kwa bei inayolipika ikiwa kama mtaji uliopangiliwa haukutolewa kwa kiwanda, kwenye meli, katika reli na kwa jeshi la watu waliofunzwa kuviendesha. Unaweza kupata picha kidogo juu ya umuhimu wa mtaji uliopangiliwa kwa kujaribu kufikiria wewe mwenyewe kama uliye na mzigo wa jukumu la kukusanya na kutoa kifungua kinywa rahisi kwa familia ya mjini iliyotajwa hapo juu pasipo msaada wa mtaji.

Kupata chai ungepaswa kufanya safari ya China au India. Ikiwa kama wewe siyo muogeleaji mahiri, ungeliweza kuchoka hata kabla ya kwenda na kurudi. Halafu tatizo jingine lingeweza kukukumba. Ungeliweza kutumia nini badala ya pesa hata kama ungelikuwa imara kuogelea baharini?

Kupata sukari ungepaswa kuogelea umbali mwingine mrefu kwenda visiwa vya Caribbean, au matembezi marefu kwenda mashamba ya viazi sukari. Lakini hata hivyo ungeliweza kurudi bila sukari kwasababu jitihada zilizopangiliwa na pesa ni muhimu kuzalisha sukari, bila kusema chochote juu ya kinachohitajika kusafisha, kusafirisha na kuifikisha kwenye meza ya kifungua kinywa.

Mayai ungeweza kuyapata kirahisi vya kutosha lakini ungeweza kutembea umbali mrefu sana kabla hujaweza kupata glasi mbili za juisi ya chungwa. Ungepaswa kutembea umbali mwingine mrefu mpaka kwenye mashamba yanayolimwa ngano kupata vipande viwili vya mkate wa ngano. Nafaka  ingeliweza kuondolewa kutoka kwenye menyu kwasababu isingeweza kupatikana isipokuwa kwa kutumia nguvu za ushirika wa watu waliofunzwa na mfumo unaofaa, vyote vikihitaji mtaji.

Wakati ukiwa umepumzika, ungeweza kuanza safari nyingine ya kuogelea kushuka chini kuelekea Amerika ya Kusini ambapo ungeweza kuchukua ndizi kadhaa na wakati ukirudi ungeliweza kutembea kidogo kuelekea shamba la ng’ombe wa maziwa na kuchukua siagi na jibini kidogo. Hatimaye familia yako jijini ingeliweza kuwa tayari kuketi chini na kufurahia kifungua kinywa.

Inaonekana kama upuuzi, au siyo?

Vizuri, njia iliyoelezwa ndiyo ambayo  ingeliweza kuwa njia pekee inayowezekana bidhaa hizo rahisi za chakula kuweza kupatikana katikati ya jiji ikiwa hatukuwa na mfumo wa Kibepari.

Jumla ya pesa zilizohitajika kwa ajili ya kujengea, kuendeleza reli na meli zilizotumika katika usafirishaji wa kifungua kinywa hicho rahisi ni nyingi kiasi cha kuduwaza akili ya mtu. Hufikia mamia ya mamilioni ya dola bila ya kutaja  jeshi la wafanyakazi wenye ujuzi waliohitajika kuendesha meli na treni hizo. Lakini usafirishaji ni sehemu tu ya mahitaji ya ustaarabu wa kisasa.

Kabla hakujaweza kuwa na kitu chochote cha kusafirisha, kitu fulani ni lazima kipandwe ardhini kwanza, au kuzalishwa na kutayarishwa kwa ajili ya soko. Hii huhitaji mamilioni ya dola zaidi kwa ajili ya vifaa, mitambo, ufungashaji, masoko, na kwa ajili ya mishahara ya mamilioni ya wanaume na wanawake. Meli na barabara za garimoshi havimei tu kutoka ardhini na kufanya kazi moja kwa moja. Huja baada ya mwito wa ustaarabu, kupitia nguvukazi na uadilifu na uwezo wa kupangilia wa watu walio na ubunifu, imani, shauku, maamuzi na uvumilivu!  Watu hawa hujulikana kama mabepari(Wajasiriamali). Wanatiwa ari kwa shauku ya kujenga, kutengeneza, kutimiza, kutoa huduma zenye manufaa, kupata faida na kukusanya utajiri. Na kwasababu wanatoa huduma ambazo bila hizo kusingelikuwa na ustaarabu, wanajiweka wenyewe katika njia ya utajiri mkubwa.

Kuweka tu kumbukumbu kwa urahisi na zinazoeleweka, nitaongeza kwamba hawa mabepari(wajasiriamali) ndio watu walewale ambao wengi wetu tumesikia wasemaji kwenye majukwaa wakiwataja. Ni watu walewale ambao wenye misimamo mikali, walanguzi, wanasiasa wasio waaminifu na viongozi wa vyama vya wafanyakazi  huwaita “Wanyang’anyi”

Sijaribu kutetea au kupinga kundi lolote la watu au mfumo wowote wa kiuchumi. Sijaribu kushutumu majadiliano ya jumla pale ninapotaja ‘Viongozi wa ushirika’ wala sina lengo la kuwapatia hati safi watu wote waitwao mabepari.

Lengo la kitabu hiki – lengo ambalo kwa uaminifu nimejitolea zaidi ya robo karne nikiwasilisha kwa wale wote wanaotaka maarifa, filosofia ya kutegemewa zaidi ambayo kupitia hiyo watu wanaweza kupata utajiri kwa kiasi chochote kile wanachotamani.


Hapa nimechanganua faida za kiuchumi za mfumo wa kibepari kwa malengo mawili ya kuonyesha,

1.  Kwamba wote wale wanaotafuta utajiri ni lazima watambue na kuendana wenyewe na mfumo unaodhibiti njia zote za utajiri uwe mkubwa au mdogo na
2.  Kwamba ni lazima wawe upande wa picha kinyume na ule unaoonyeshwa na wanasiasa na wafitini ambao huchukulia kupangilia mtaji kana kwamba ni kitu chenye sumu.

............................................................................

Ndugu msomaji wa tafsiri ya kitabu hiki cha Think & Grow Rich(Fikiri Utajirike), usikose sehemu ya mwisho ya Sura hii ya 7 siku ya Alhamisi. Pia ikiwa hukutuma namba yako kwa ajili ya kujiunga na kundi la Whatsapp la Semina za michanganuo ya biashara za kipekee mwaka huu, basi bado hujachelewa tuma ujumbe kwa whatsapp, namba 0765553030 ukisema 'NIUNGANISHE NA KUNDI LA WASSAP LA MICHANGANUO' 


 SOMA SURA NA SEHEMU ZILIZOPITA HAPA

0 Response to "PESA BILA AKILI NI HATARI, NI NYENZO KUBWA YA MAFANIKIO IKITUMIKA VIZURI"

Post a Comment