MAAJABU YALIYOLETA BARAKA ZOTE HIZI KATIKA UCHUMI WA KIMAGHARIBI | JIFUNZE UJASIRIAMALI

MAAJABU YALIYOLETA BARAKA ZOTE HIZI KATIKA UCHUMI WA KIMAGHARIBI



Jitathmini wewe Mwenyewe
Maswali 28 Unayopaswa Kujibu

Tathmini ya mwaka ni muhimu katika kutafuta soko la huduma kikamilifu kama ilivyokuwa katika tathmini ya mwaka kwa bidhaa. Na zaidi, tathmini ya mwaka inatakiwa ibainishe kupungua kwa makosa na kuongezeka kwa mema. Mtu husonga mbele, kusimama pale alipo au kurudi nyuma katika maisha. Lengo la mtu linapaswa bila shaka liwe ni kusonga mbele. Tathmini ya mwaka itabainisha ikiwa hatua imepigwa, na kama hivyo ndivyo, ni kwa kiasi gani. Itabainisha pia hatua zozote zilizopigwa kurudi nyuma mtu anazoweza kuwa amepiga.Utafutaji kikamilifu wa soko la huduma humtaka mtu kupiga hatua hata kama maendeleo ni ya taratibu.

Tathmini yako ya mwaka inapaswa kufanywa mwishoni mwa kila mwaka kusudi uweze kujumuisha katika maazimio yako ya mwaka mpya maboresho yeyote ambayo tathmini inaonyesha yanatakiwa kufanywa. Fanya tathmini hii kwa kujiuliza mwenyewe maswali yafuatayo na kuhakikisha usahihi wa majibu yako kwa msaada wa mtu mwingine ambaye hatakuruhusu kujidanganya mwenyewe.

Maswali ya tathmini binafsi kwa ajili ya kujichunguza.
1. Nimetimiza kile nilichoazimia kama lengo langu kwa mwaka huu?(Unapaswa kufanya kazi na lengo la mwaka lililokuwa dhahiri litakalotimizwa kama sehemu ya lengo lako kubwa la maisha .

2. Nimetoa huduma katika ubora wa hali ya juu kabisa ambao nilikuwa na uwezo nao au ningeliweza kuboresha zaidi sehemu yeyote ya huduma hizi?

3. Nimetoa huduma kwa kiasi kikubwa kadiri inavyowezekana nilichokuwa na uwezo nacho?

4. Dhamira ya matendo yangu imekuwa linganifu na shirikishi muda wote?

5. Nimeruhusu tabia ya kuahirisha kupunguza ufanisi wangu, na kama ndiyo ni kwa kiasi gani?

6. Nimeboresha haiba yangu, na kama ndiyo ni kwa njia zipi?

7. Nimekuwa na msimamo katika kufuatilia mipango yangu?

8. Nimefikia maamuzi mara moja na kwa ukamilifu katika matukio yote?

9. Nimeruhusu hofu yeyote au zaidi ya zile hofu sita za msingi (angalia sura ya 15), kupunguza ufanisi wangu?

10. Nimekuwa aidha muangalifu kupita kiasi au muangalifu chini ya kiasi?

11. Uhusiano wangu na wenzangu kazini umekuwa mzuri au mbaya ? kama umekuwa mbaya, kosa ni la kwangu kwa sehemu au ni la kwangu lote?

12. Nimetawanya nguvu zangu zozote kupitia kukosa umakini wa kukusanya nguvu sehemu moja?

13. Nimekuwa muelewa na mvumilivu katika mambo yote?

14. Ni katika njia ipi nimeboresha uwezo wangu wa kutoa huduma?

15. Nimekuwa mlafi katika tabia zangu zozote?

16. Nimejieleza aidha kwa uwazi au kwa siri, aina yeyote ya majivuno?

17. Matendo yangu kwa wenzangu yamekuwa ni ya kuwashawishi kuniheshimu?

18. Maoni yangu na maamuzi yamekuwa yakizingatia utabiri au usahihi wa tathmini na fikra?

19. Nimekuwa nikifuata tabia ya kuweka bajeti ya muda wangu, matumizi yangu, na kipato changu na nimekuwa nikizilinda bajeti hizi?

20.Ni muda kisi gani nimepoteza katika juhudi zisizokuwa na faida, ambao ningeliweza kuutumia kwa faida zaidi?

21. Nawezaje kubajeti upya muda angu na kubadilisha tabia zangu kusudi niwe na ufanisi zaidi katika mwaka unaokuja?

22. Nimekuwa na hatia ya tendo lolote ambalo halikupitishwa na dhamira yangu?

23. Ni kwa njia zipi nimetoa huduma bora na nyingi zaidi kuliko nilivyolipwa?

24. Sijatenda haki kwa mtu yeyote, na ikiwa ndiyo ni kwa namna gani?
 
25. Ikiwa ningekuwa mnunuzi wa huduma zangu mwenyewe kwa mwaka mzima, ningeliweza kuridhika na ununuzi wangu ?

26. Mnunuzi wa huduma zangu anaridhika na huduma nilizotoa, na kama siyo, kwanini siyo?

27. Nipo kwenye shughuli sahihi, na kama siyo ni kwanini?

28. Kiwango changu katika kanuni za msingi za mafanikio ni kipi?(fanya tathmini hii bila upendeleo kwa ukweli, na mpe mtu mwingine aipitie ambaye ni jasiri vya kutosha kuifanya kwa usahihi).

Baada ya kusoma na kushika taarifa zilizomo humu kwenye hii sura, sasa upo tayari kutengeneza mpango wa kivitendo kwa ajili ya  kutafuta soko la huduma zako. Wale waliopoteza mali zao na wale ambao ndio kwanza wanaanza kutafuta pesa, hawana chochote isipokuwa kuzitoa huduma zao kwa malipo ya utajiri. Kwa hiyo ni muhimu kwamba wanazo tayari taarifa za kivitendo  zinazohitajika kutafuta soko la huduma zao kwa faida nzuri kabisa.

Taarifa zilizomo katika sura hizi zitakuwa za manufaa makubwa kwa wale wote wanaotamani kushika uongozi katika nyanja yeyote. Itakuwa msaada hasahasa kwa wale wanaolenga kutafuta soko la huduma zao kama biashara au watendaji wakuu wa viwanda.

Kushiriki moja kwa moja na kuelewa juu ya taarifa zilizoelezwa hapa kutakuwa msaada katika kutafuta soko la huduma za mtu, na pia kutamsaidia mtu kuwa mchanganuzi na mwenye uwezo wa kuhoji watu. Taarifa zitakuwa na thamani isiyopimika kwa wakuu wa utumishi, mameneja utumishi na watendaji wengine wenye majukumu ya kuchagua wafanyakazi na ya kutunza ufanisi wa taasisi. Kama una mashaka na kauli hii, ufanyie uhakiki kwa kujibu katika maandishi maswali 28 ya kujitathmini binafsi. Kwa kweli , hilo linaweza kuwa jambo la kuvutia na wakati huhuo lenye faida hata kama hautilii mashaka ukamilifu wa kauli hiyo.


Wapi na ni kwa jinsi gani Unaweza kupata Fursa za kupata Utajiri
Sasa tayari tumechanganua kanuni ambazo utajiri unaweza kupatikana, kwa asili tunauliza hivi, “ Ni wapi mtu anaweza kupata fursa zinazofaa kutumia hizi kanuni?” Vizuri sana, ngoja tufanye uchunguzi na kuona ni nini uchumi wa Kimagharibi unaweza kumpa mtu anayetafuta utajiri mkubwa au mdogo.

Kwa kuanza, tukumbuke sote kwamba tunaishi katika jamii ambamo kila raia mwema anafurahia uhuru wa mawazo na uhuru wa vitendo. Wengi wetu hatujawahi kamwe kuchunguza faida za uhuru huu. Hatujawahi kuulinganisha uhuru wetu usiokuwa na mipaka na uhuru uliominywa katika baadhi ya jamii nyingine.

Hapa tuna uhuru wa mawazo, uhuru wa kuchagua na kufurahia elimu, uhuru katika dini, uhuru katika siasa, uhuru katika uchaguzi wa biashara, taaluma au kazi, uhuru wa kujikusanyia na kumiliki bila kunyanganywa mali zote tunazoweza kukusanya, uhuru wa kuchagua sehemu zetu za kuishi, uhuru katika ndoa, uhuru kupitia fursa sawa kwa makabila yote, uhuru wa kusafiri, uhuru katika uchaguzi wetu wa vyakula na uhuru wa kulenga kwenye hatua yeyote maishani ambayo tumejiandaa wenyewe. Tuna aina nyingine za uhuru, lakini orodha hii itatoa mtazamo wa jumla wa juu (mtazamo wa jicho la ndege) muhimu zaidi ambao unajumuisha fursa ya kiwango cha hali ya juu kabisa.

Kisha ngoja tuhesabu tena baadhi ya baraka ambazo uhuru wetu mpana umeweka mikononi mwetu. Chukua familia ya kawaida katika jamii ya Kimagharibi kwa mfano(maana yake familia ya kipato cha kawaida) na jumuisha faida zinazopatikana kwa kila mwanafamilia.

·       CHAKULA. Kutokana na uhuru wetu kwa watu wote familia ya kawaida mpaka mlamgoni mwake inao uchaguzi wa chakula, na katika bei iliyo ndani ya uwezo wake kiuchumi.

·       MALAZI.  Familia hii huishi katika nyumba bora, iliyo na gesi kwa ajili ya kupasha joto, umeme, pamoja na gesi kwa ajili ya kupikia. Mkate kwa ajili ya kifungua kinywa umeokwa kwenye jiko la umeme, kapeti husafishwa kwa mashine(vacuum cleaner) inayoendeshwa kwa umeme. Maji ya moto na ya baridi yanapatikana muda wote jikoni na bafuni. Chakula huhifadhiwa na baridi katika jokofu linaloendeshwa kwa umeme. Mke hutengeneza nywele zake, kufua nguo zake na kuzinyoosha kwa pasi ya umeme iliyo rahisi kutumia kwenye nguvu ya umeme inayopatikana kwa kupachika plagi ukutani. Mume hunyoa ndevu kwa kutumia mashine ya umeme. Wanapata burudani kutoka pande zote za dunia, masaa 24 kwa siku ikiwa watataka, kwa kitendo cha kuwasha tu luninga zao.

·       MAVAZI. Wanaume na wanawake katika jamii za Kimagharibi wanaweza kupata mahitaji yao ya mavazi na kuvaa bila wasiwasi kwa bei mshahara wa familia ya kawaida unaoweza kumudu.


Ni mahitaji ya msingi matatu tu ya chakula, mavazi na malazi yaliyotajwa. Raia wa kawaida anazo stahili zingine na faida anazopata kwa malipo ya jitihada za wastani zisizozidi masaa manane kwa siku ya kazi. Miongoni mwake ni stahili ya kumiliki gari, ambalo mtu anaweza akatoka na kurudi kwa hiyari yake kwa gharama kidogo sana.

 Ukipenda kusoma sura zote zilizowekwa


……………………………………………


Ndugu msomaji usikose sehemu ya sita ya sura hii ya 7 siku ya Jumatatu. Pia niombe radhi kwa kutotimiza uzinduzi wa kundi la Whatsapp la semina za michanganuo pamoja na semina yenyewe ya kuchanganua miradi ya kiubunifu iliyokuwa na uwezo mkubwa wa kuzalisha faida haraka kama nilivyoahidi. 

Sababu kubwa ni maandalizi ya group lenyewe lakini karibu litakamilika naomba tuvute subira kidogo kwa wale waliokwisha jiunga. Kwa wale ambao bado hawajajiunga nafasi bado ipo wazi KARIBUNI SANA! Tuma ujumbe wa “NIUNGANISHE KUNDI LA WASAP SEMINA ZA MICHANGANUO” namba yetu wassap ni 0765553030

Wahi pia offa ya vitabu vitatu 3 vya self help books katika mfumo wa softcopy kwa bei ya sh 15,000/= badala ya elfu 18,000/= kabla haijamalizika tarehe 10 mwezi huu. Tuma pesa kwenye 0712202244  au  0765553030 jina Peter Augustino Tarimo utatumiwa vitabu muda huohuo.






0 Response to "MAAJABU YALIYOLETA BARAKA ZOTE HIZI KATIKA UCHUMI WA KIMAGHARIBI"

Post a Comment