BAADA YA MASOMO 11 SEMINA YA MPANGO WA BIASHARA SASA INAINGIA AWAMU YA PILI | JIFUNZE UJASIRIAMALI

BAADA YA MASOMO 11 SEMINA YA MPANGO WA BIASHARA SASA INAINGIA AWAMU YA PILI


Awamu ya kwanza ya masomo ya semina ya jinsi ya kuandika mchanganuo wa biashara ilijumuisha vitu hivi vifuatavyo,

·       Utambulisho wa semina,
·       Masomo ya msingi 11 katika mifumo ya PDF na mp3,
·       Violezo(Templates)
·       vitabu vya michanganuo ya biashara, kile cha kiswahili cha “MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI” pamoja na kitabu kingine maarufu sana duniani cha namna ya kuandika mpango wa biashara katika lugha ya kiingerera kimoja.
·       Pamoja na masomo mengine kadhaa ya ziada.

Masomo hayo yalikuwa yakitolewa kwa njia ya BLOGU HII MAALUMU(kuingia ni kwa aliyelipia tu) ambayo wasomaji wake huingia baada ya kulipa kiingilio cha Tsh. 10,000/=. Masomo yote katika PDF na mp3 hutumwa pia kwa njia ya email kusudi mshiriki aweze kudumu nayo muda wote hata ikiwa hatadownload ama kusoma masomo yaliyopo katika blogu hiyo.

SOMA: Jinsi ya kujiunga na Semina ya michanganuo ya biashara.

Katika kipindi kisichopungua miezi mitatu, semina hii walijiunga watu wengi na waliweza kujifunza masomo ya semina huku wengi wakitoa mirejesho mbalimbali kama vile kuuliza maswali kwa mambo ambayo hawakuyaelewa vizuri, kutoa maoni mbalimbali ya namna ya kuboresha semina na hata wengine kuchangia mada mbalimbali kwa njia za email, meseji na kisanduku cha maoni.

Baada ya awamu hiyo wadau wengi walipendekeza kuwa ikiwezekana tuanze awamu nyingine ambayo ‘itadili’ zaidi na uandishi wa moja kwa moja(kwa vitendo zaidi) wa michanganuo ya biashara huku msisitizo ukiwa katika kipengele au sehemu ya fedha ambayo kwa mujibu wa wadau wengi wanasema ndiyo kipengele kigumu kuliko vingine vyote.

Mwanzoni tulikuwa tumepanga kwamba mshiriki wa semina atahesabu amehitimu semina hii baada ya kuweza yeye mwenyewe kuandika mpango wa biashara yake atakayoipenda, na tulifikiri kuwa kila mshiriki aliyeanza semina siku zile za mwanzo mpaka kufikia mwezi huu wa nne tayari angekuwa ameshamaliza kuandika mchanganuo huo. Hata hivyo washiriki asilimia kubwa wameshakamilisha lakini bado wapo baadhi ambao hawajakamilisha.

SOMA: Huna muda wa kutosha kuandika mpango wa biashara?

Kutokana na maoni ya washiriki hata na wale walioweza tayari kuandika michanganuo yao, tumeona umuhimu wa kuwa na awamu ya pili ya semina hiyo itakayozingatia zaidi maeneo hayo mawili lakini pia hata na maeneo yale ambayo mshiriki mmoja mmoja atakuwa hajayaelewa vizuri.

Tutaanza kuchambua na kuandika michanganuo ya biashara mbalimbali kuanzia mwazo mpaka mwisho huku tukionyesha hatua kwa hatua jinsi kila kipengele kinavyoandikwa. Sambamba na hilo pia tutaweka msisitizo zaidi katika kipengele au sehemu ya makisio ya fedha. Masomo yatawekwa asubuhi au jioni na mchanganuo mmoja utachukua siku tatu kumalizika.

Tutaanza awamu ya pili ya semina kwa kuchanganua mpango wa biashara ya saluni sehemu za biashara, bidhaa/huduma, uongozi, na mikakati siku ya kwanza, kisha soko siku ya pili na kumalizia na sehemu ya fedha siku ya 3. Hata hivyo katika michanganuo mingine kwenye awamu zitakazofuata, tutaanza na kipengele chochote ili kuthibitisha kuwa unapoandika mpango wako wa biashara hulazimiki kufuata mlolongo wa vipengele/sehemu jinsi ulivyokuwa rasmi bali unaanza popote isipokuwa muhtasari tu unaokuwa wa mwisho mara zote.

Kwa washiriki wanaoendelea kujiunga kuanzia sasa wasiwe na wasiwasi wowote kwamba wamechelewa kwani watajifunza kila kitu ambacho wenzao waliotangulia walijifunza kutokana na mfumo wa semina yenyewe kuw ni ule wenye kunyumbulika(flexible)

Mfumo wa semina hii ni ule ambao masomo yake yote na kila kitu kinachofundishwa hurekodiwa katika hii BLOGU MAALUMU YA MASOMO YA SEMINA YA MICHANGANUO, ambayo ipo muda wote kwa mshiriki yeyote aliyetoa kiingilio cha shilingi elfu 10 pamoja na kututumia anuani yake ya baruapepe(email) aina ya GMAIL ambayo ndiyo tunayoitumia kumtumia mwaliko wa kujiunga na blogu hiyo. Kisha yeye hubonyeza  kiungo(link) itakayotumwa kwenye email yake na tayari sasa atakuwa akiingia katika BLOGU hiyo kila anapohitaji bila kikwazo.

Kwa washiriki wale wa zamani waliotangulia kujiunga, nao wasiwe na hofu hata kidogo kwani watakwenda sambamba na hao wapya huku wakijifunza kwa undani zaidi kivitendo pamoja na kujipiga msasa katika maeneo yale ambayo hawakuyamudu vyema, lengo likiwa ni “kumaster” kabisa uandaaji wa mpango wa biashara.
……………………………………………………………….......

KWA MAWASILIANO NA MRATIBU WA SEMINA AU KUJIUNGA NA SEMINA HII, TUMIA NAMBA ZA SIMU ZIFUATAZO,

0712 202244   AU  0765 553030
Jina: Peter Augustino Tarimo


0 Response to "BAADA YA MASOMO 11 SEMINA YA MPANGO WA BIASHARA SASA INAINGIA AWAMU YA PILI"

Post a Comment