UKWELI HUU WA MAISHA UNAUMA LAKINI UNAWEZA KUUBADILISHA KABLA YA KUFA-2 | JIFUNZE UJASIRIAMALI

UKWELI HUU WA MAISHA UNAUMA LAKINI UNAWEZA KUUBADILISHA KABLA YA KUFA-2


Katika makala iliyopita iliyokuwa ikisema, UKWELI MCHUNGUKILA MTU ANAOPASWA KUUKUBALI MAISHANI KABLA YA KUIAGA DUNIA, mwishoni mwa makala ile niliahidi kwamba sehemu ya pili ya makala hiyo itaendelea na tutaona ni nini suluhisho la hali hii ambayo imekuwa ni kama sheria kwamba binadamu kama anavyozaliwa mwenyewe akiwa peke yake basi na anapofikia hatua ya kuzeeka basi hana budi kubakia tena mpweke na mwishowe hata kufa akiwa peke yake pasipo hata watu wake wa karibu kama watoto wajukuu au mwenza kuwa nae karibu.

Wenzetu wazungu imefikia hatua mbaya zaidi kwani mtu akishazeeka hupelekwa katika vituo vya kulelea wazee ambako anakwenda kuishi na wazee wenzake. Hali hii ililetwa na maendeleo ya binadamu, kukua kwa miji na utandawazi kwani ukiangalia vizazi vya huko nyuma sana hakukuwa na kitu cha namna hii, wazee waliishi na watoto wao, wajukuu na hata vitukuu mpaka wanakufa wakiwa na furaha na amani ya kutosha.

SOMA: Njia za kujiingizia pesa(kipato) nje ya kazi yako ukiwa umeajiriwa au una biashara nyingine.

Kitu kikubwa tena kinachochangia hali hii ya wazee kutokuthaminika tena ni maisha ya kutafuta pesa, fedha imekuwa ndiyo kila kitu, watoto wanapokua na kumaliza shule huamua kwenda kuishi mijini na kuwaacha wazazi wakiendelea kuishi vijijini wenyewe. Hata mijini nako utakuta wazee wengi hutelekezwa na watoto wao huku wao wakielekezea nguvu zao nyingi kwa familia zao na kwa kuwa hali za maisha kwa watu wengi ni ngumu na kipato ni kidogo hakitoshelezi mahitaji ya kila siku ya familia, utakuta wazazi wakiachwa wajitegemee wenyewe. Sasa kama hgivyo ndivyo watu waache kutafuta pesa?

SULUHISHO.
Suluhisho pekee la tatizo hili ni kuboreshwa kwa hali za kiuchumi miongoni mwa jamii zetu pamoja na kuhimiza maadili mema kwa watoto, kuwaheshimu wazazi pamoja na kumcha Mungu katika dini zetu. Pesa ni lazima iendelee kutafutwa. Hali ya kiuchumi ni suala nyeti sana, watu wengi siyo kama wanapenda kuishi mijini au mbali na wazazi kwa miaka mingi pasipo kuwaona, ni kutokana na hali mbaya ya kiuchumi, kipato kisichokidhi mahitaji pamoja umasikini ndivyo vitu vikubwa vinavyomfanya mtu kuwa mbali na wazazi. Utakuta mtu kila siku anakuwa na matumaini kwamba siku moja atafanikiwa, lakini miaka inasonga mbele bila ya mafanikio yeyote na ndipo hukuta mtu anazidi  kukaa.

Kujikwamua kiuchumi hakuna njia ya mkato zaidi ya kuhakikisha unaongeza kipato chako, na kuongeza mapato ni lazima mtu uwe kwanza na biashara, hauwezi kamwe kuboresha hali yako ya kiuchumi pasipo kuwa na biashara, haiwezekani kabisa!. Biashara hapa namaanisha shughuli zozote zile za kiuchumi zinazolenga kutengeneza faida. Katika kitabu cha MIFEREJI 7 YA PESA unapoanza tu kukisoma utakutana na sura inayoelezea shughuli za namna hiyo. Kumiliki biashara peke yake hakuwezi kutosha kukukwamua kiuchumi ndani ya muda mfupi,unahitaji pia kutumia mbinu mbalimbali za kijasiriamali ambazo kwa kiasi kikubwa kabisa zimezungumziwa katika kitabu kingine cha MICHANGANUO YA BIASHARANA UJASIRIAMALI.

Na zaidi ya hapo unatakiwa pia kujiwekea mifereji 7 ya pesa au kwa maana nyingine mifereji 7 ya kipato ambayo nayo imefafanuliwa kwa kina katika kitabu hicho. Mifereji hii sasa ndiyo itakayokuhakikishia wewe uwezo wa kufanya lolote lile bila ya kuzuiwa na kikwazo chochote kile cha pesa, unaweza ukasafiri hata ikiwa ni mara 2 kwa wiki kwenda kijijini kuwaona ndugu na jamaa zako, unaweza ukawachukua ndugu na jamaa zako hususan wazazi wako na kwenda kuishi nao popote pale duniani na kuwarudisha myumbani muda wowote watakaohitaji wao bila ya kuhofia nauli utatoa wapi nk.

Self Help Books tunayo Package nzima(kifurushi) ambacho ni suluhisho kwa mtu yeyote anayetaka kuachana na umasikini kwa muda mfupi. Ukipata kitabu chetu kimoja cha bure kiitwacho, KANUNI NA SIRI YA KUJIFUNZAELIMU YA PESA NA MAFANIKIO, halafu ukaja kusoma na vitabu vitatu vilivyopo hapa kwenye picha chini ama hata kama utavikosa basi angalao ujitahidi kupata hicho cha Michanganuo ya biashara na ujasiriamali, utakuwa huna haja tena ya kuhangaika, kama utaamua kusoma aina nyingine za vitabu vya pesa na mafanikio basi itakuwa tu ni kwa ajili ya marudio au kujiburudisha.

Sasa ukishaamua kumiliki biashara yeyote ile  na nafikiri uamuzi wa ni biashara ipi itakufaa utaupata baada ya kupitia vitabu hivyo au hata kama tayari unao ujuzi wa kulitambua wazo zuri la biashara inayokufaa. Kumbuka biashara inaweza kuwa hata ya kilimo, ufugaji, uvuvi, biashara ya rejareja, biashara ya jumla au biashara nyingine yeyote ile.

Chagua wazo la biashara iliyokuwa na uwezo wa kukuinua haraka kwa mfano, angalia ni kitu/vitu gani ambavyo watu wanavihitaji sana na kuna dalili kuwa mahitaji hayo yataendelea kudumu kwa kipindi kirefu kijacho, hapa mimi ijapokuwa kwa watu wengine wanaweza kuona ni biashara kichaa lakini mimi nasema biashara kama ya duka la rejareja mahitaji yake kwa watu/raia ni endelevu na hakuna dalili yeyote kwamba kutakuwa na mdororo wa maduka hayo kwa kipindi chochote kijacho.

Wazo jingine ni biashara ya kilimo cha mazao ya chakula na mifugo. Unaweza ukamuona mtu anayehamia shamba leo kuwa ni kama chizi vile, lakini kama ni mtu siriazi kamcheki baada ya miaka miwili au mitatu utakuta siyo mwenzako tena! Kufuga wanyama na ndege, kila siku watu wanatamani kula nyama na hamna siku watu wataacha kupenda nyama na vyakula vyenye jamii ya protini ya wanyama kwani miili ya watu inavihitaji vitu hivyo kila kukicha. Kikubwa hapa tu ni maarifa sahihi ya namna ya kudili navyo vikupe faida na maarifa hayo si mengie bali ni haya haya ya biashara na ujasiriamali. (Pata mchanganuo wa ufugaji wa kuku 1000 wa mayai toka kwetu kwa bei rahisi kabisa)

Wazo hilo lenye uwezo wa kukuinua haraka anza kulifanyia kazi kikamilifu bila kuchelewa, husisha watu wengine mfano wanafamilia au wasaidizi utakaoamua kuwalipa ujira, tafuta mtaji wa kutosha na hakikisha mtaji huo unaulinda zaidi ya mboni ya jicho lako kwani bila mtaji wa kueleweka hautakuwa tofauti na mtu anayelima kwa jembe lisilokuwa na mpini, simamia kikamilifu mapato yako usikubali yahujumiwe kwa njia yeyote ile(Usicheke na kima utavuna mabua)

Kwa kifupi tu, hivyo ndivyo utakavyoweza kubadilisha jadi na sheria zilizozoeleka tu lakini hazina ukweli wowote. Ukiwa ni mtu mwenye nguvu kiuchumi mambo mengi yanayodhaniwa kuwa hayawezekani kwako yatawezekana, ni mambo machache sana yatakayokushinda yakiwemo kweli yale ambayo Mwenyezi Mungu ameyaweka kama vile kuugua, kufa nk. lakini siyo vitu eti kama kuwatunza wazazi ama wazee wa familia ambao nao walitoa mchango wao mkubwa katika kukufanya wewe leo hii uwe kama ulivyo. 

SOMA: Maajabu ya kufikiri mambo makubwa maishani.

Kujijengea uwezo mkubwa wa kiuchumi hakuna njia nyingine zaidi ya hizi hizi zinazoelezwa na wataalamu mbalimbali, lakini kubwa zaidi ni kuzingatia sana hesabu hii muhimu kuliko zote katika biashara ambayo inapatikana kwenye kitabu cha MIFEREJI 7 YA PESA NA SIRI MATAJIRI WASIYOPENDA KUITOA toleo jipya 2016/2017

Soma: sehemu ya kwanza 1 ya makala hii hapa.

Dr. Remmy Ongala mwimbaji maarufu nchini Tanzania aliwahi kusimulia kupitia wimbo wake huu, No money No Life, hakuna pesa, hakuna maisha, akisisitiza jinsi ambavyo maisha bila kuwa na uchumi imara yanavyoweza kuwa magumu, alimwita bwana mdogo wake hivi, ampelekee salamu kwa wazazi kijijini;

Peleka salamu zangu nyumbani kijijini mwambie baba na mama kwamba bado nasota.....maisha mjini maanayake pesa zaidi......pesa, pesa inapeleka watu jela...........Maisha bila pesa ni kama adhabu, hakuna heshima, kama huna pesa utapata tabu, huwezi kula, huwezi kuoga wala huwezi kulala....pesa, pesa inaleta maneno....kila mtu anahitaji pesa......

Remmy Ongala wimbo(audio) no money no life,


Bado hujajiunga na SEMINA ya michanganuo ya biashara? Jiunge sasa hivi bado hujachelewa, ni shilingi 10,000/= nafasi ni chache.

0 Response to "UKWELI HUU WA MAISHA UNAUMA LAKINI UNAWEZA KUUBADILISHA KABLA YA KUFA-2"

Post a Comment