WASANII WA VIDEO NA FILAMU TANZANIA: TEKNOLOJIA HII ITAWATOA KIMASOMASO | JIFUNZE UJASIRIAMALI

WASANII WA VIDEO NA FILAMU TANZANIA: TEKNOLOJIA HII ITAWATOA KIMASOMASO


Ili kusambaza filamu za Kiafrika, video za muziki, vipindi vya watoto, pamoja na show mbalimbali za televisheni kutoka Afrika kupitia kifaa
maalunu kiitwacho “Tango box” au king’amuzi cha Tango, televisheni huunganishwa na mtandao wa intaneti yenye 3G wifi. Humpa nafasi mtazamaji kutazama filamu na video za muziki zote zilizoko mtandaoni mahali popote pale panapotatikana intaneti ya simu za mkononi.

Waanzilishi wa kampuni hii ni vijana watatu wajasiriamali na wabunifu kutoka Tanzania, Victor Joseph Mnyawani, Peter Khamis Siniga na Moses Kabungo chini ya udhamini wa Tume ya sayansi na teknoloja ya Tanzania. Victor Joseph mmoja wa waanzilishi akiongea na Idhaa ya Kiswahili ya  redio ‘Deutsche welle’ Ujeruani alisema kuwa , Tango TV ni huduma ya kusambaza filamu sanasana za Kitanzania na za Kiafrika kwa ajili ya Waafrika.

Alisema, wametengeneza mfumo wa kusambaza filamu kwa njia ya intaneti ambapo king’amuzi hicho kiitwacho Tango huunganishwa kwenye televisheni ya kawaida na mtu kupata filamu za kitanzania, mpya na zile za muda uliopita, filamu hizo unazipata hapohapo bila ya kusubiri wala kwenda kununua DVD au VCD.

Akielezea tofauti iliyokuwepo kati ya Tango tv na zile filamu au video za bure za kwenye youtube ambazo watu wengi hupendelea kutumia ‘youtubedownloader’ kuzifungua, alisema kwamba, kweli kwenye intaneti zipo video za bure lakini pia zipo zile video na filamu ambazo huwezi ukazipata bure, na wasanii wanaziuza kwa njia ya DVD na VCD

“Wale watengeneza filamu tutakaoingia nao mikataba hawataweka filamu zao bure katika mtandao wa youtube” Alisema. Kwa upande wa gharama, Kabungo alisema Mtanzania wa kawaida atamudu. Ni kwamba bei zao zinaridhisha, kibox(king’amuzi) cha Tango ambacho ndicho huunganisha intaneti na televisheni wanakiuza shilingi laki moja, 100,000/= na kila filamu kwa wastani inagharimu sh. 3,000/- na ukishailipia filamu hiyo itabakia kwenye king’amuzi huku ukiwa na uwezo wa kuitazama muda wowote ule upendao, ila tu huwezi ukaitoa na kuisambaza kwa mtu mwingine mithili ya watu wanavyo burn CD na DVD kiholela.

Kabungo anaendelea kusema kuwa hamna gharama kubwa kwa mtu akishakuwa na TV yake, wao humpa king’amuzi pamoja na rimoti(remote) ya televisheni. Hutumia cable aina mbili, zile za kawaida za ‘AV’ na ambazo zilikuwa pia zikitumika katika TV za analojia, na zile za ‘HDMI’ ambazo hutumika sasa na ni za kidijitali zaidi.

Kwa upande wa soko la Tango TV, alisema ni kubwa sana kutokana na sababu kwamba matumizi ya intaneti nayo yameongezeka sambamba na gharama zake kushuka na hii inatokana na uwekezaji mkubwa katika miundombinu “infrastructure”  ya mawasiliano na watu nao siku hizi wanapendelea zaidi kutazama filamu za Kitanzania na za Kiafrika.

Wazo hili lilitoka wapi?
Victor, mmoja wa waanzilishi anasema, wazo hili mwanzoni kabisa lilitokana na alipokuwa chuoni alipobaini tatizo kubwa kwenye usambazaji wa filamu za Kitanzania, watengenezaji wa filamu walikuwa wakilalamika kwamba hawatengenezi fedha za kutosha kwenye filamu zao, kusambaza kwa DVD ni gharama na wao hawana mtaji wa kutosha.Pia tatizo jingine ni utengenezaji wa DVD na CD feki tatizo linalowanyima mapato mengi sana.
Vijana watatu (3) wa Kitanzania, wabunifu na waanzilishi wa teknolojia ya kusambaza filamu ya Tango TV.

Waliangalia pia tatizo la watu wengi kutokuwa na kompyuta japo wanazo simu za mikononi lakini hawapendi kutazama filamu ndefu kwenye simu. Kwa hiyo wakapata wazo kuwa ukiwawezesha watu kuunganisha intaneti na televisheni zao, itakuwa rahisi zaidi kwao kupata filamu wanazozitaka na pia itawarahisishia wale watengeneza filamu kuongeza njia mpya ya kutengeneza pesa.

Ili kutumia filamu na video za wasanii mbalimbali Tango wanafanya mikataba ya kibiashara na wamiliki wa kazi hizo. Vile vile wametengeneza ushirika na  tasnia husika kwa kuanzisha ushirikiano na Shirikisho la Filamu Tanzania TAFF.

Rais wa Shirikisho la filamu Tanzania, Simon Mwasamba alisema huduma ya Tango itasaidia sana kupunguza “piracy” (wizi wa filamu kwa njia zisizokuwa halali) “Unatoa movie yako leo, wewe kabla hujafika Mwanza, movie yako imeshafika Mwanza” alisema Mwasamba. Kupitia teknolojia hii ya Tango tv, “kukopi itakuwa haiwezekani”.

Naye mtengenezaji na mtayarishaji wa filamu, bwana John Kalege  anasema kwamba awali alidhani kuwa teknolojia inachangia kudumaza sanaa lakini alikuja kutanabahi kuwa sanaa ni lazima pia iende na wakati.



Vijana hawa watatu waliiambia “Deutsche welle” kwamba wanatarajia kupanua zaidi biashara yao na kuzijumuisha nchi nyingine za Afrika ya Mashariki zikiwemo, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi. Vie vile walisema watajaribu kuzijumuisha na sinema/filamu za Ki Nigeria.

Mahojiano hayo kati ya waanzilishi wa Tango TV na Redio Ujerumani yasikilize hapa chini;

0 Response to "WASANII WA VIDEO NA FILAMU TANZANIA: TEKNOLOJIA HII ITAWATOA KIMASOMASO"

Post a Comment