UNAWALINDAJE WATOTO WADOGO POPOTE PALE ULIPO NA MABAYA? | JIFUNZE UJASIRIAMALI

UNAWALINDAJE WATOTO WADOGO POPOTE PALE ULIPO NA MABAYA?


Tukiwa leo hii tarehe 12 june tukiadhimisha siku ya Umoja wa Mataifa ya kupinga kutumikishwa watoto wadogo na ajira mbaya, yafaa kila mpenda utu Duniani kujiuliza ni kwa namna gani popote pale ulipo iwe ni nyumbani kwako, barabarani, kazini na hata safarini jinsi unavyoweza kushiriki katika kuzuia mateso kwa watoto wadogo.

Masikini kundi hili la watu haliwezi kujitetea lenyewe. Hata ikiwa mtoto atapata mateso makalikiasi gani, mfano ni yule mtoto wa boksi, ni vigumu sana kujitetea, huumia kimya kimya mpaka anakufa, labda tu atokee msamaria atakayebaini hali hiyo na kumuokoa.

Sasa kila mtu angehakikisha katika mazingira anamoishi ama kufanya kazi anakuwa mlinzi wa mtoto, maharamia wanaowadhulumu wasingelipata nafasi kwani wangeripotiwa mapema kwenye jamii husika na vyombo vya usalama kabla hali haijawa mbaya zaidi kwa mtoto husika.
 
AJIRA KWA WATOTO WADOGO
Ikumbukwe kuwa mtoto siyo lazima awe anaonekana na umbile dogo kama wa miaka 2 au 3, watoto wengine hasa wale wa kike utakuta wana maumbile makubwa jambo linalosababisha ‘mijibaba’ hasa ile miroho na isiyokuwa na chembe ya huruma kudhania ni wakubwa wenzao na kuanza kuwahadaa ili kuwaingiza katika mambo mbalimbali ya kikubwa iwe ni mapenzi, kazi ama hata kuwatamkia maneno yasiyostahili katika umri wao.


Tuache ile tabia ya kudai eti “Mtoto wa mwenzio siyo wa kwako bali ni mkubwa mwenzio”  Kabla haujamtumikisha mtoto wa mwenzio katika mazingira magumu au kumtendea unyama wa kutisha, hebu kwanza jiulize kama angelikuwa ni wa kwako je, ungeliridhika Tu afanyiwe hivyo?

0 Response to "UNAWALINDAJE WATOTO WADOGO POPOTE PALE ULIPO NA MABAYA?"

Post a Comment