FOLENI SASA BASI: USAFIRI BINAFSI NA DALADALA ZA ANGANI ZINAKUJA JE, UMEJIANDAA? | JIFUNZE UJASIRIAMALI

FOLENI SASA BASI: USAFIRI BINAFSI NA DALADALA ZA ANGANI ZINAKUJA JE, UMEJIANDAA?

Kutokana na shida kubwa ya usafiri katika majiji makubwa kama vile Dar es salaam, kuna wakati mtu unakaa ndani ya daladala na kutamani kama kungelikuwa na usafiri wako binafsi  wa angani ambao hakuna foleni ambayo ingekuzuia".
 
Usafiri wa angani na nchi kavu, nusu gari nusu ndege.
Teknolojia ya usafiri wa chombo ambacho nusu ni gari na nusu ni ndege, haipo mbali tena, Professa katika taasisi ya teknolojia ya anga ya Massachusset anasema hivi, “Tunakoelekea kutakuwa na usafiri binafsi wa anga ambao nusu ni gari na nusu ni ndege, ni mchanganyiko wa ndege zisizokuwa na rubani zinazoendeshwa kwa kompyuta ‘Drones’ na magari ya roboti, hivyo ndege yako pia itakuwa ndiyo gari lako”

“Ijapokuwa ndege za drones zinapigiwa sana kelele na vyombo vya habari, lakini ukweli ni kwamba mtu unaposafiri kwa ndege ya kawaida  ni sawa sawa na unasafiri ukiwa  katika Drone. Usafiri siku za baadae angani  na nchi kavu utakuwa salama zaidi na ikiwa matumizi ya kompyuta yatatumika kwa kiasi kikubwa. Hamna kikwazo kikubwa kiteknolojia katika kufikia ndoto hizo, zaidi ya vikwazo vya kisaikolojia na kitamaduni katika watu kuachana na usafiri wa magari ya kawaida.


Chanzo BBC

1 Response to "FOLENI SASA BASI: USAFIRI BINAFSI NA DALADALA ZA ANGANI ZINAKUJA JE, UMEJIANDAA?"

  1. Bora uje tu maana shida tunayopata hasa sisi tunaokaa mbali kama huku mbezi inatisha

    ReplyDelete