NI WATU WENYE KINGA DHIDI YA WOGA NA VIPOFU WA KUSHINDWA JAMBO WANALOANZISHA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

NI WATU WENYE KINGA DHIDI YA WOGA NA VIPOFU WA KUSHINDWA JAMBO WANALOANZISHA

think & grow rich sura ya 8iii

Maoni kuhusiana na tabia ya mtu huyu inaonekana kutokuwa na umuhimu. Ni lazima ieleweke kwa kila mtu anayesoma ujumbe huu wa kushangaza kwamba ni mtumaji wa ujumbe mwenye uaminifu wa kiwango cha juu kabisa. Hili ni muhimu. (Ni walaghai na wanasiasa wasiowaaminifu waliotumia vibaya madaraka yao ndio maana watu kama kina Adams walikufa).

Gavana Gage alipopokea majibu ya kuchoma ya Adams, alipandwa na ghadhabu na kutoa tangazo lililosomeka , “Hapa kwa jina la Mfalme, natoa na kuahidi msamaha wake mkubwa kwa watu wote watakaoweka silaha zao chini mara moja na kurudi katika jukumu la mazungumzo ya amani isipokuwa tu wasiohusika na msamaha huo ni, Samuel Adams na John Hancock ambao upinzani wao ni wa kihalifu mno mtu kukubali uamuzi mwingine wowote zaidi ya adhabu kali.”

Kama ambavyo mtu anaweza akasema katika lugha ya siku hizi, Adams na Hancock walikuwa kwenye, ‘shabaha’ Kitisho cha Gavana aliyekasirika kiliwalazimisha  watu hao wawili  kufikia uamuzi mwingine wenye hatari inayolingana na ule wa kwanza. Haraka waliitisha mkutano wa siri na wafuasi wao imara (Hapa kushauriana kulianza kuchukua hatua) Bada ya mkutano kuwa umeanza, Adams alifunga mlango akaweka funguo katika mifuko yake na kuwaambia wote waliokuwemo kwamba ilikuwa ni muhimu Baraza la Makoloni kuundwa na hivyo  hakuna mtu atakayeruhusiwa kutoka nje ya chumba mpaka uamuzi kwa ajili ya baraza hilo umefikiwa.

Mshangao mkubwa ulifuata. Baadhi walipima matokeo yanayoweza kutokea ya uasi wa namna hiyo(woga) Wengine walielezea hisia zao za mashaka makubwa kuhusiana na busara ya uamuzi mkubwa kiasi hicho wa kuonyesha upinzani kwa ufalme. Walikuwa wamejifungia mle ndani watu wawili walio na kinga ya woga, vipofu wa uwezekano wa kushindwa. Hancock na Adams. Kupitia ushawishi wa akili zao, wengine walivutika kukubali kwamba, kupitia kamati ya mahusiano, mipango ni lazima ifanyike kwa ajili ya mkutano wa baraza la kwanza la Bara utakaofanyika Philadelphia Septemba 5 1774.

Kumbuka tarehe hii, ni muhimu kuliko July 4 1776. Ikiwa kama kusingelikuwa na uamuzi wa kufanya mkutano wa Bara, kusingeliweza kuwa na kusaini tangazo la Uhuru. Kabla ya kikao cha kwanza cha Baraza jipya, kiongozi mwingine, katika eneo jingine la nchi alikuwa amezama katika mapambano ya kuchapisha Muhtasari wa Haki za Koloni la Uingereza Marekani.

Alikuwa ni Thomas Jefferson wa jimbo la Virginia ambaye uhusiano wake na Lord Dunmore(mwakilishi wa Mfalme Virginia) ulikuwa umezorota kama ule wa Hancock na Adams na Gavana wao. Mara tu baada ya Muhtasari maarufu wa haki kuchapishwa, Jefferson alijulishwa kwamba alikuwa anakabiliwa na mashtaka ya uhaini mkubwa dhidi ya Serikali ya Mtukufu Mfalme.

Akiguswa na hilo tishio, mmoja wa washirika wa Jefferson, Patrick Henry, kwa uwazi alitamka yaliyokuwa akilini mwake, alihitimisha mapendekezo yake kwa sentensi itakayobakia kuwa mashuhuri milele, ‘Ikiwa huu ni uhaini, basi ufanye kuwa zaidi’ Ilikuwa ni watu kama hawa, bila ya nguvu, bila madaraka, bila ya nguvu za kijeshi, bila pesa, waliketi kwa taadhima wakifikiria hatima ya makoloni, wakianza katika ufunguzi wa Baraza la kwanza la Kibara(continental congress), na kuendelea katika muda wa kila baada ya miaka miwili mpaka tarehe 7 June 1776, Richard Henry Lee aliposimama akahutubia kiti, na kwa mshangao Baraza lilitoa  hoja hii;

“Waungwana, natoa hoja kwamba Umoja huu wa Makoloni ni huru na yana haki ya kuwa huru na majimbo yanayojitegemea, kwamba yanasamehewa kutokana na tuhuma zote kwa ufalme wa Uingereza, na kwamba uhusiano wote wa kisiasa kati yao na Taifa la Uingereza umevunjwa na unapaswa kuvunjwa kabisa”  


Hoja ya kushangaza ya Lee ilijadiliwa kwa hamasa na kwa kirefu kiasi kwamba alianza kukosa subira. 



0 Response to "NI WATU WENYE KINGA DHIDI YA WOGA NA VIPOFU WA KUSHINDWA JAMBO WANALOANZISHA"

Post a Comment