PROGRAMU YA KOMPYUTA INAYOTUMIA TWITTER KUPIMA HISIA ZA WATU YAGUNDULIWA. | JIFUNZE UJASIRIAMALI

PROGRAMU YA KOMPYUTA INAYOTUMIA TWITTER KUPIMA HISIA ZA WATU YAGUNDULIWA.

Wanasayansi wa Kiingereza wamegundua programu ya kompyuta ambayo wanadai inao uwezo wa kupima hisia za wananchi katika Taifa kwa kutumia mtandao wa kijamii wa Twitter. Programu hiyo waliyoiita “EMOTIVE” inafanya kazi kwa kutathmini mawazo ya mihemko yanayotumwa katika mtandao huo wa kijamii.


Wamesema ina uwezo wa ‘ku-scann’ (kupitia) mpaka ‘tweets’(mawazo) 2,000 kwa sekunde moja na kuyatolea majibu ikiwa wananchi hao wapo katika hali ya hasira, chuki, huzuni ama furaha. Wanadai ‘Emotions’ itasaidia katika kukabiliana na vurugu za kiraia na kutabiri mapema tishio la usalama wa umma.
 
Zaidi ya watu million 500 duniani kote wanatumia Twitter, na zaidi ya ‘tweets’(jumbe) 340 milioni hutumwa kila siku. Profesa  John Jackson , aliyeongoza utafiti huo  alisema, jamii kutumia mitandao ya kijamii kuelezea mawazo yao huonyesha kwa usahihi na kwa wakati kile watu wanachofikiria.

Naye Dr.Ann O Brien mshiriki mwingine alisema, “Kwa tukio lolote lile tunaweza kuona jinsi mwitikio unavyoongezeka na kupungua kwa muda fulani”

Mfumo huu kwa sasa unatumika kupima tweets(jumbe) nchini Uingereza peke yake, lakini watafiti hao wamesema, baadaye wataweza kuuboresha zaidi kupima tweets Duniani kote.


Na, BBC

0 Response to "PROGRAMU YA KOMPYUTA INAYOTUMIA TWITTER KUPIMA HISIA ZA WATU YAGUNDULIWA."

Post a Comment