Ndani ya Programu yetu ya MAKE YOUR SELF GREAT AGAIN wiki iliyomalizika jana tulikuwa na zoezi zito la kuanzisha Usomaji wa kitabu Maarufu cha Think & Grow Rich.
Namshukuru Mungu zoezi limeenda vizuri na mpaka kufikia
leo hii tumeshamaliza kusoma sura ya pili japo tunakwenda kwa mwendo wa
kinyonga kidogo kwa lengo hasa la kutokuwaacha nyuma wenzetu wenye kasi ndogo
ya usomaji.
Programu yetu tulisema itakuwa na vitu vingi ndani yake
lakini kubwa zaidi ikiwa ni Mafunzo ya kina juu ya uandaaji wa Michanganuo ya
biashara (Business planning).
Kwanini business planning? Ni kwa sababu mpango wa
biashara ni kila kitu, ndani yake utakutana na vipengele vingine vyote
vinavyounda biashara mfano masoko, mauzo, usimamizi, uongozi, fedha na kila
kitu kingine kinachofanya biashara iitwe biashara.Tunaua ndege wote kwa jiwe
moja!
Hivyo kuanzia Jumatatu ya tarehe 4/7/2025 tutaendelea na
zoezi la mafunzo ya uandishi wa Michanganuo ya biashara hatua kwa hatua kwa
vitendo na sasa badala ya kuwa na mchanganuo wa biashara moja tu wa kufundishia
tutakuwa nayo mitatu (3). Hii inamaanisha kwamba tutakuwa na madarasa matatu
tofauti yakiendelea kwa wakati mmoja
Unapojiunga sasa unakuwa na fursa ya kuchagua ni mchanganuo wa biashara ipi utapenda kujifunzia, tunayo michanganuo ya biashara za aina nyingi ikiwemo michanganuo ya kuku, mgahawa, saloon, utengenezaji wa sabuni, duka la rejareja, kilimo cha tikiti maji, uokaji wa keki na vitafunwa, biashara ya genge, ufyatuaji tofali za saruji na mingine mingi
Mafunzo haya ya semina yataendeshwa kwa mfumo wa maandishi/text
watsap, voice notes, videos na PDF
Mwisho wa kujiunga na madarasa kwa wiki hii ni Alhamisi,
watakaojiunga Jumanne, Jumatano na Alhamisi watajifunza mafunzo yaliyotangulia
kwa muda maalumu ili waweze kulingana na wenzao waliowahi. Kujiunga zaidi ya Alhamisi
itabidi mtu asubiri madarasa ya wiki zinazofuata.
JINSI
YA KUJIUNGA NA KIINGILIO
Ada ya mwaka ni Tsh. 20,000/= lakini ukiwahi kabla ya
offa kuisha unalipia Tsh. 10,000/=
tu
HUDUMA ZETU NYINGINE MBALIMBALI ZA MALIPO
(VITABU & MICHANGANUO YA BIASHARA)
1. Kuandikiwa Mchanganuo wa Biashara yako
Tunaandika Mpango kamili wa biashara yeyote ile kwa Kampuni na wafanyabiashara binafsi kwa gharama rafiki, njoo tuzungumze kupitia namba za simu au wasap 0765553030 / 0761002125 Michanganuo yetu tunaandaa kulingana na maono ya mteja kama yalivyo pamoja na mazingira ya soko linalomzunguka
2. Kitabu cha MAFANIKIO YA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA
Kitabu hiki kilichowasaidia wajasiriamali wengi wadogo na wale wa kati kinatatua changamoto mbalimballi za biashara za rejareja kubwa ikiwa ni usimamizi wa mapato yasipotee au kudokolewa kiholela na wasaidizi wako, ni uzoefu wa zaidi ya miaka 12 wa mwandishi mwenyewe kwenye hii biashara.
Kukipata unaweza ukatembelea duka letu la mtandaoni kukinunua hapo kwa kiungo hiki>>MAFANIKIO YA BIASHARA DUKA LA REJAREJA
3. Kitabu cha THINK & GROW RICH –SWAHILI EDITION (FIKIRI & UTAJIRIKE)
Kitabu hiki kilichosomwa duniani na zaidi ya watu milioni 100 tunayo nakala ya Kiswahili kwa bei zifuatazo;
Ukiwa popote pale Duniani unaweza kukipata kwenye mtandao wa GETVALUE kupitia kiungo hicho kibofye kuingia ununue sasa hivi na kukidownload.
4. Vitabu zaidi &Michanganuo mbalimbali ya biashara
Kwa vitabu zaidi na Michanganuo mbalimbali ya biashara iliyo tayari tembelea duka letu hili la mtandaoni uweze kuona na kujinunulia kwa urahisi kabisa>>SELF HELP TANZANIA ONLINE BOOSHOP

0 Response to "SEMINA NA MAFUNZO: JINSI YA KUANDIKA MICHANGANUO YA BIASHARA KIVITENDO YAANZA TENA WIKI HII KWA KISHINDO!"
Post a Comment