HUDUMA ZETU

HUDUMA ZETU

HUDUMA NA BIDHAA MBALIMBALI TUNAZOZITOA:
Self Help Books pamoja na kuuza vitabu vya aina mbalimbali pia tunatoa na huduma nyinginezo kama ifuatavyo;


1. VITABU VYA BIASHARA NA UJASIRIAMALI

1.  Michanganuo ya Biashara na Ujasiriamali sh. 30,000/= Hardcopy (cha karatasi ) na 10,000 softcopy kwa email

2.  Siri ya mafanikio ya Biashara Duka la Rejareja sh. 15,000/= cha karatasi na 6,000/= softcopy

3.  Mifereji ya Pesa na Siri Matajiri wasiyopenda kuitoa sh. 5,000/= cha karatasi na 3,000/= softcopy

3.  Fikiri na Utajirike (THINK & GROW RICH-SWAHILI-EDITION) hardcopy ni Tsh. 27,000/= tunampelekea mteja alipo Dar es salaam na Mikoani kwa mabasi ni shilingi 35,000/= E-book yake unaweza kujipatia kupitia mtandao huu hapa wa>>> GETVALUE


*Ukitaka vitabu/kitabu kama upo Dar es salaa, wasiliana na sisi na utaletewa kitabu/vitabu mpaka mahali ulipo)

   *Mikoani kwa basi tunatuma kwa uaminifu mkubwa na hakuna hatari ya mteja kupoteza fedha zake kwani tunabeba dhamana kwa hatari yeyote inayoweza kutoke njiani .

   *Vitabu kwa njia ya mtandao(E-Books) kama softcopy ukilipia tunatuma ndani ya dakika 5.


2. KUNDI LA WHATSAP NA TELEGRAM

Tuna kundi la watsap liitwalo MICHANGANUO ONLINE MASTER MIND GROUP pamoja na Channel ya Telegram.
 
Kiingilio ni shilingi 10,000/= kwa muda wa mwaka mmoja tokea siku ya kujiunga na  ukishalipa mara moja unapata tiketi ya kushiriki semina na masomo yote yatakayotolewa katika group. 

Masomo yanalenga hasa hasa Michanganuo bunifu ya biashara zinazolipa Tanzania, Jinsi ya kuongeza mzunguko wako mwenyewe wa fedha na kwenye biashara yako. Ikiwa hutumii whatsapp bado utapata masomo kama kawaida kupitia email yako.

Katika masomo na Semina zetu unapata pia fursa mbalimbali pamoja na vitu adimu kabisa ambavyo ni spesho kwa wale waliojiunga tu. Kuna vitu kama elimu maalumu binafsi ya fedha(Special personal cashflow management) pamoja na mbinu za kuboresha mtiririko wa fedha kwa ujumla katika biashara ambazo ndiyo nyenzo muhimu kabisa katika kuamua mtu ufanikiwe au usifanikiwe.


3. USHAURI KWA WAJASIRIAMALI WADOGO NA WALE WANAOAZA BIASHARA

1.  Ushauri mfupi mfupi kwa njia za meseji, simu au wasap kwa wajasiriamali wadogowadogo hasa wale wanaoanza. Huduma hii kwa sasa hivi ni bure, hatuchaji gharama yeyote.



RATIBA YA UWEKAJI MAKALA KILA SIKU

(a) Makala zinaendelea mfululizo(series)
Kila siku
Makala za kawaida na ushauri 






4. HUDUMA YA KUANDIKIWA MCHANGANUO WA BIASHARA
Kwa anayehitaji huduma ya kuandikiwa mchanganuo wa biashara yake (BUSINESS PLAN) iwe mpya au ya zamani, tunatoa huduma hiyo kwa usahihi na kwa muda mfupi inavyowezekana.  

Kazi hiyo huchukua siku 2  mpaka wiki moja kulingana na ukubwa wa biashara na taarifa zilizopo tayari. Gharama kwa biashara za mtaji wa chini ya sh.milioni 10 ni sh. 100,000/= na kwa biiashara za mtaji wa zaidi ya sh. milioni 10 gharama ni asilimia 1% ya mtaji wa biashara husika. 

Gharama hizi ni kwa michanganuo ya biashara aina zote, uwe ni wa kuombea fedha au ni kwa ajili ya kuendeshea tu biashara yako, na mteja hutoa advance nusu ya fedha kisha kuja kumalizia kazi inapokamilika.

Mteja huchagua ni lugha ipi itumike, kiswahili ama kiingereza  katika kuandika mchanganuo wa biashara yake. Mchangnuo huwa na vipengele vyote muhimu au kulingana na matakwa ya mteja mwenyewe.

Hatufanyi kopy & Paste ya michanganuo iliyokwishaandikwa tayari bali tunaandika mchanganuo mpya(fresh) kulingana na mazingira ya biashara ya mteja pamoja na mahitaji yake, ndio maana michanganuo yetu huwa hatutumii masaa au siku moja tu kuikamilisha, ni kuanzia siku 2 mpaka wiki moja na kuendelea kuegemeana na upatikanaji wa taarifa muhimu za utafiti wa biashara husika.

Tofauti na kwingine, makisio ya hesabu katika michanganuo yetu ni kwa miaka 3 - 5 na kuendelea na siyo miezi 6 tu au mwaka mmoja peke yake, na tunaweka ripoti zote tatu muhimu za mahesabu kamili, Faida na Hasara (Projected Profit and Loss), Mtiririko wa Fedha Taslimu (Projected Cash flow) na Mizania ya Biashara (Projected Balance Sheet). Tunaweka pia makisio ya ripoti hizo miezi yote 12 ya mwaka wa kwanza pamoja na Uwiano au sehemu muhimu za biashara hiyo.

*Aidha tunafanya makisio ya hesabu kwa mpango wa biashara ambao mteja anakuwa amekwishaandika tayari sehemu nyinginezo lakini bado hajakamilisha kipengele cha Fedha. Gharama ni ndogo zaidi kulinganisha na kuandika mchanganuo mzima kila kitu. 



Karibu sana upate huduma bora kabisa, semina na vitabu kwa gharama nafuu uboreshe biashara na maisha yako kwa ujumla.

Mwalimu/Mhamasishaji na mwandishi wako.
Peter A. Tarimo

SIMU /  WHATSAPP:              0712 202244  /   0765 553030
   

8 Responses to "HUDUMA ZETU"

  1. hata ushauri ni lazima uulipie kwanza!!!??

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hapana, soma vizuri pale juu, ushauri mfupi usiozidi dakika 15 ni bure kabisa, hatujawahi kumchaji mtu. Pia unaweza kuuliza maswali kupitia nnjia nyinginezo kama meseji, email au wasap.

      Delete
  2. Mbna najaribu kudownload vitabu nashindwa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni mpaka ujiunge(Usubscribe) pale kwenye box juu kwa anuani yako ya email, majina na namba ya simu hatimaye utadownload vitabu vyako bila wasiwasi wowote ule.

      Delete
  3. Mbna najaribu kudownload vitabu nashindwa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Jiunge kwa email pale kwenye box juu utadownload.

      Delete