IKIWA KWELI UNATAKA MAFANIKIO, UDHAIFU HUU NI LAZIMA UUKWEPE | JIFUNZE UJASIRIAMALI

IKIWA KWELI UNATAKA MAFANIKIO, UDHAIFU HUU NI LAZIMA UUKWEPE


THINK AND GROW RICH SURA YA 9 SEHEMU YA NNE
Dalili za Ukosefu wa Uvumilivu
Hapa utakuta adui wa kweli wanaosimama katikati yako na mafanikio ya maana. Hapa hautakutana tu na dalili zinazoonyesha mapungufu ya msimamo, bali pia sababu za ndani kabisa katika ufahamu wa ndani za udhaifu huu. Isome orodha kwa uangalifu na ukubali mwenyewe kwa uaminifu KAMA KWELI UNATAKA KUFAHAMU WEWE NI NANI NA NI NINI UNACHOWEZA KUKIFANYA. Haya ni madhaifu ambayo ni lazima yadhibitiwe na wale wote wanaotafuta utajiri.

1.  Kushindwa kutambua na kuelezea kwa ufasaha hasa kile unachotaka.

2.  Kuahirisha kwa sababu au bila sababu(mara nyingi kukisaidiwa na jeshi la kutisha la visingizio na udhuru)

3.  Kukosa moyo wa kujifunza ujuzi maalumu

4.  Kukosa uamuzi, “tabia ya kukwepa wajibu” katika matukio yote badala ya kukabiliana na mambo kwa ukweli (pia kukisaidiwa na visingizio)

5.  Tabia ya kutegemea visingizio badala ya mipango kamili kwa ajili ya kutatua matatizo

6.  Kuridhika binafsi. Ipo dawa lakini kidogo sana kwa ajili ya tabia hii na hakuna matumaini kwa wale wanaosumbuliwa nayo.

7.  Kutokujali, kwa kawaida huakisiwa katika utayari wako wa kukubaliana katika matukio yote, kuliko kukutana na upinzani na kupambana nao.

8.  Tabia ya kuwalaumu wengine kwa makosa yako na kukubali mazingira yasiyofaa kama kwamba hayaepukiki.

9.  Udhaifu katika shauku unaotokana na kutokujali kwenye uchaguzi wa sababu zinazochochea vitendo.

10.          Utayari hata wa hamu ya kujitoa katika dalili za mwanzo za kushindwa (kunakotegemea moja au zaidi ya hofu sita za msingi)

11.          Ukosefu wa mipango iliyoratibiwa, kuwekwa katika maandishi ambapo inaweza ikachanganuliwa.

12.          Tabia ya kupuuzia kusogelea mawazo au kudaka fursa wakati inapojitokeza yenyewe.

13.          Kutamani badala ya kudhamiria.

14.          Tabia ya kukubaliana na umasikini badala ya kulenga katika utajiri – ukosefu wa jumla wa shauku ya kuwa, kutenda na kumiliki.

15.          Kutafuta aina zote za njia za mkato za kupata utajiri, kujaribu kupata pasipo kutoa kiasi kinacholingana, mara nyingi huakisiwa katika tabia ya kucheza kamari au jitihada za kufanya majadiliano ‘makali’ ya bei.

16.          Hofu ya kukosolewa, kushindwa kutengeneza mipango na kuiweka katika vitendo kwa sababu ya kile watu wengine wanachofikiria kufanya au kusema. Adui huyu hukaa mwanzoni mwa orodha, kwa sababu hukaa kwa ujumla katika akili ya ndani pasipo kushitukiwa (tazama hofu sita za msingi katika Sura ya 15)

Hebu tuzikague baadhi ya dalili za hofu ya kukosolewa. Wengi wa watu huruhusu ndugu, marafiki na jamii kwa ujumla kuwaathiri kiasi kwamba hawawezi kuishi maisha yao kwa sababu huogopa kukosolewa.

Idadi kubwa ya watu hufanya makosa kwenye ndoa, hutimiza makubaliano na kuingia maisha ya mateso na huzuni  kwasababu wanahofia ukosoaji unaoweza kufuata ikiwa watarekebisha makosa (Mtu yeyote aliyejiweka chini ya aia hii ya hofu anafahamu uharibifu usiorekebishika inaoufanya kwa kuharibu malengo, kujitegemea na shauku ya kufanikiwa)

Mamilioni ya watu hudharau kupata elimu ya ziada baada ya kuwa wamemaliza shule kwasababu wanahofia ukosoaji. Idadi isiyohesabika ya wanaume na wanawake wote wadogo kwa wakubwa huruhusu ndugu kuharibu maisha yao  kwa kisingizio cha wajibu kwa sababu huogopa ukosoaji (wajibu haumhitaji mtu yeyote kujisalimisha katika uharibifu wa malengo yao binafsi na haki ya kuishi maisha yao katika njia zao wenyewe)

Watu hukataa kuchukua hatari kwenye biashara kwa sababu wanaogopa ukosoaji unaoweza kufuata ikiwa watafeli. Woga wa ukosoaji katika mambo hayo una nguvu kuliko shauku ya mafanikio. Watu wengi sana hukataa kujiwekea malengo makubwa, au hata kupuuzia kuchagua ajira kwasababu wanahofia ukosoaji wa ndugu na marafiki wanaoweza kusema, “usiwe na malengo makubwa hivyo watu watafikiria umechanganyikiwa”

Wakati Andrew Carnegie alipopendekeza kwamba, nijitolee miaka 20 kwa ajili ya ukusanyaji wa falsafa ya mafanikio ya mtu, msukumo wangu wa kwanza wa fikra ulikuwa ni hofu ya kitu gani watu wangeweza kusema. Pendekezo liliweka lengo kwa ajili yangu lisilolingana kabisa na lengo jingine lolote nililowahi kuwa nalo. Kwa haraka kama mwanga wa tochi, akili yangu ilianza kujenga visingizio na sababu, zote zikiwa na dalili za hofu ya asili ya ukosoaji.

Kitu ndani yangu kilikiniambia, “Hautaweza kuifanya- kazi hiyo ni kubwa mno na inahitaji muda mwingi mno – ndugu zako watakufikiriaje? Utaendeshaje maisha yako?

Hakuna mtu aliyewahi kuanzisha falsafa ya mafanikio hivyo unayo haki gani ya kuamini unaweza kufanya? Wewe ni nani kwa vyovyote  kuwa na malengo makubwa kiasi hicho? Kumbuka kuzaliwa kwako masikini. Unaelewa nini kuhusu falsafa? Watu watafikiri umechanganyikiwa akili(na walifanya hivyo). Kwanini watu wengine hawajawahi kufanya hivi kabla ya sasa?”

Haya na maswali mengine mengi yalimulika katika akili yangu na kutaka majibu. Ilionekana kama kwamba Dunia yote ilikuwa imenigeukia ghafla  kwa lengo la kunidhihaki ili niachane na shauku yote ya kutekeleza pendekezo la Bwana Carnegie. Nilikuwa na fursa iliyokuwa wazi muda uleule ya kuiua nia kabla haijaniongoza.


 SOMA SURA NA SEHEMU ZOTE ZILIZOPITA HAPA



0 Response to "IKIWA KWELI UNATAKA MAFANIKIO, UDHAIFU HUU NI LAZIMA UUKWEPE"

Post a Comment