KILA MWANAMKE MJASIRIAMALI HUKUTANA NA CHANGAMOTO HIZI KUBWA 4 KWENYE SAFARI YAKE | JIFUNZE UJASIRIAMALI

KILA MWANAMKE MJASIRIAMALI HUKUTANA NA CHANGAMOTO HIZI KUBWA 4 KWENYE SAFARI YAKE

CHANGAMOTO ZA MWANAMKE MJASIRIAMALI

Ni jambo la kutia moyo sana siku hizi kuona idadi ya wanawake wanaoingia kwenye ujasiriamali au kuanzisha biashara zao ikiongezeka kwa kwa kasi ya kuridhisha. Na ongezeko hilo la wanawake wajasiriamali halionekani hapa Tanzania tu bali Afrika Mashariki nzima na Dunia kwa ujumla.




Lakini hata hivyo mwelekeo huu wa kutia moyo kusema ukweli haumaanishi kwamba ndio wanawake na wanaume sasa wana uwanja uliokuwa sawia kwa asilimia mia moja kwenye sekta ya ujasiriamali. Bado zipo changamoto mahsusi zinazoendelea kuwakwaza wanawake kwasababu tu wao ni wanawake. Bila ya kupoteza muda mwingi hebu moja kwa moja tuzione hizo changamoto;


1.VIKWAZO KATIKA KUVIFIKIA VYOMBO VINAVYOTOA MIKOPO NA MITAJI

Mfumo dume uliokita mizizi karibu katika kila sekta ya maisha kwenye jamii, sekta ya fedha nayo haijasalimika. Taasisi nyingi za kifedha au zile zinazokopesha wajasiriamali wadogo na wakubwa zimetawaliwa kwa kiasi kikubwa na wanaume ambao ndio watoaji maamuzi muhimu. Na kwa bahati mbaya sana wanaume hao wengi hawako tayari kabisa kuwaona wanawake wakipata fursa sawa na wao.



Matokeo yake wanawake hujikuta katika nyakati ngumu wanapogundua kwamba hawapewi umuhimu unaostahili pale wanapokwenda kutafuta au kuomba mikopo kwa ajili ya kukuzia biashara zao. Wanawke wanajikuta wakiendelea kufanya ujasiriamali na mtaji mdogo waliokuwa nao jambo linalowazuia wasione mafanikio ya haraka kama ilivyo kwa wenzao wanaume. Namna ya kukuza mtaji imekuwa ni changamoto ya kwanza mjasiriamali mwanamke anayokutana nayo wakati akifikiria jinsi ya kuwa mjasiriamali.


2.UNYANYASWAJI KIJINSIA.

Changamoto hii ndiyo iliyokuwa ikipewa kipaumbele kikubwa zaidi na vyombo mbalimbli vya habari kote duniani hasa hasa katika zile nchi zilizoendelea kiasi cha kufikia hatua ya watu wengi maarufu kama wasanii na waigizaji wa sinema wakubwa kule Hollywood Marekani wakajikuta wakiwajibika kwa vitendo vyao vya ukatili wa kijinsia walivyokuwa wamezowea kuwafanyia mabinti wanaokwenda katika kiwanda hicho cha filamu Hollywood kusaka umaarufu.



Hizo ni habari njema hata hapa Tanzania tunapaswa kuiga mfano. Unyanyasaji wa kijinsia upo karibu katika kila sekta kuanzia sekta za burudani, siasa, media, fedha nk. na wanawake mara zote ndio ambao wamekuwa wahanga wa ukandamizaji huo. Unyanyasaji wa kijinsia una sura nyingi kuanzia unyanyasaji kwa kutumia maneno kama vile matusi na maneno ya kuvunja moyo, kunyimwa fursa, vipigo na hata kulazimishwa kufanya vitendo vya mapenzi bila ridhaa ya mwanamke mwenyewe.


3.UWIANO BAINA YA BIASHARA NA FAMILIA

Siyo wanawake wajasiriamali tu peke yao wanaokumbana na changamoto hii bali hata na wale wanawake walioko kwenye ajira pia na wao hili huwasumbua sana. Kubalansi muda wa kulea watoto na familia wakati huohuo wakihakikisha biashara au kazi inaendelea vizuri ni mtihani mkubwa na kwa mwanamke hili huwa gumu zaidi kutokana na sababu kwamba jamii hasa zile za Kiafrika zimejijengea kasumba kwamba kazi za kulea familia ni spesho tu kwa mwanamke. Waswahili husema mshika mawili moja humponyoka, mwanamke inabidi achague kwa wakati ule aliopo ni kipi muhimu zaidi ya kingine, kwa mfano ana mtoto mchanga itambidi kwanza biashara aiweke pembeni au amtafute mlezi.



4.KUKOSA UUNGWAJI MKONO

Hii hasahasa ni kwa wanawake wale walioko katika nafasi za juu kama mameneja, viongozi nk. wakati mwingine hujikuta wapweke sana kwani ni vigumu zaidi kwao kupata wanawake wenzao wa kuiga mfano(mentors) kutokana na idadi ya wanawake waliokuwa juu kuwashinda wao kuwa ndogo mno nah ii imetokana na sekta nyingi nafasi za juu kutawaliwa n wanaume ambao kama kawaida yao wengi hawapendi kuwaona wanawake wakiwa katika nafasi za maamuzi kama wao au juu kuwashinda.


Angalau siku hizi wanawake kidogo kidogo wanaanza kutapa nafuu kutokana na ujio wa mitandao ya kijamii ambapo wanawake wenyewe wanakuwa na uwezo wa kuwasiliana na wanawake wenzao hata walioko mbali kutiana moyo ili waweze kusonga mbele zaidi ikiwa ni pamoja pia na kujenga mitandao ya kibiashara.


………………………………………………………
·       Kwa vitabu bora kabisa vya ujasiriamali tembelea; SMART BOOKS TZ.

·       Kwa hudumazetu mbalimbali ikiwemo kuandikiwa mpango wa biashara yako nk. fungua, HUDUMA ZETU.

·       Kwa michanganuo maarufu 3 ya kuku aina zote(MKOMBOZI CHICKS PLAN 3PACKS) Lipia shilingi elfu 10 kupitia namba ya simu, 0712202244 utumiwe katika email yako muda huohuo. Kwa mawasiliano zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa njia ya WHATSAP namba, 0765553030      



0 Response to "KILA MWANAMKE MJASIRIAMALI HUKUTANA NA CHANGAMOTO HIZI KUBWA 4 KWENYE SAFARI YAKE"

Post a Comment