Hazijapita siku nyingi tangu Rais John Pombe Magufuli
azindue rasmi ukuta unaozuia eneo la machimbo ya madini ya Tanzanite huko
Mererani Simanjiro mkoa wa Manyara. Ukuta huo ulio na urefu wa kilomita 24 na
nusu na kimo cha mita 3 uligharimu Taifa kiasi cha shilingi bilioni 6 huku
nguvukazi iliyotumika kuujenga ikiwa ni wanajeshi wapatao 270.
Madhumuni makubwa ya kuujenga ukuta ule ni ili
kuhakikisha mapato yote yanayotokana na madini ya Tanzanite yanayosadikiwa kuwa
hayawezi kupatikana katika eneo jingine lolote lile duniani zaidi ya Tanzania
yanadhibitiwa vilivyo yasiibiwe wala kutoroshwa tena kinyemela na watu
wasiokuwa waaminifu.
Kabla ya hapo serikali ilikuwa haipati ushuru na kodi
zinazostahili kutokana na mwanya huo uliosaidia wafanyabiashara na wachimbaji
wenye tamaa ya kutajirika haraka kuficha kiasi kamili cha madini yaliyokuwa
yakichimbwa hapo mgodini.
Haikuwa nia ya makala yangu hii kuanza kuandika upya
historia ya madini haya hapa kwani hata mgunduzi wake Mzee Jumanne Mhero Ngoma
aliyeyagundua madini hayo hapo mwaka 1967 kukosa hekima za Rais Magufuli naye
chupuchupu aje afe masikini. Kwanini nasema hivyo? Nasema hivi nikitaka wewe
mjasiriamali unayesoma hapa ujue fika ya kwamba, mali zaweza kuwa ni za kwako,
biashara unaweza kuwa unaimiliki wewe mwenyewe lakini usipokuwa makini vya
kutosha katika usimamiaji wa mapato yake hakika utashanga wajanja wengine
kabisa wakinufaika na jasho lako pasipo wewe kujua mpaka pale utakapokuja
kujikuta ukifa fukara.
Si kama namlaumu mzee Ngoma wala serikali zilizopita
hapana, bali nataka tu kuonyesha umuhimu wa hatua hii iliyochukuliwa na
serikali. Nimesoma vizuri historia ya Mzee Ngoma, alikuwa na fursa nzuri sana
ya kuwa bilionea lakini alizidiwa kete na wajanja waliotumia nafasi na hata
jina lake kujinufaisha wengine mfano kama Wale wahindi waliomtapeli lile jiwe
kubwa la kwanza kabisa la Tanzanite alilookota akichunga mbuzi, mpaka hata
kesho vitukuu vyao wataishi maisha ya peponi wangali hapa duniani.
Na sisi Kama Taifa kwa upande mwingine tulikuwa na fursa
nzuri kabisa ya kunufaika na utajiri huu mkubwa toka ugunduliwe na Mzee Ngoma
miaka hiyo ya 60 lakini wajanja wachache kama makampuni kutoka nchini Kenya,
India na nchi nyinginezo ndio waliofaidi zaidi matunda hayo.
Yote hii ilitokana na kulegeza kamba katika udhibiti au
usimamizi wa rasilimali, unapolegeza kamba usipokuwa shupavu vya kutosha
wanaokukodolea ‘mimacho’ wakitamani kile ulichokuwa nacho watakichukua na
kukifanya kuwa mali yao. Hivyo nilitaka tu kukukumbusha wewe kama mjasiriamali
katika sekta hii ya usimamizi wa mali zako wewe upoje?
Ni lazima uwe king’ang’anizi wazungu husema aggressive , kuwa ng’ang’ari kwa maana
nyingine, simaanishi unyang’anye mali za watu wengine la hasha, bali namaanisha
uhakikishe unalinda vilivyo mali zako kwa gharama yeyote ile hata ikiwa ni kwa
kujenga ukuta kama huu wa Tanzanite Mererani. Wenzetu Wakenya wapo hivyo na
ndiyo maana hata makampuni yao utakuta yapo juu sana.
Binafsi baada ya kucheki sana hii mbinu aliyoibuni Rais
wetu Magufuli ya kujenga ukuta kuthibiti mapato ya Tanzanite, nilikumbuka
wakati fulani nilipokuwa naendesha biashara ya duka la rejareja niliwahi kubuni
kitu kama hiki na kwa kweli kilifanya kazi japo sikukitilia maanani sana wakati
huo mpaka majuzi nilipokuja kukumbuka na kuona si vibaya nikashea na watu
wengine nao wakakijua hususani wamiliki wa maduka ya rejareja. Kinaweza
kusaidia kwa kiasi kikubwa kudhibiti mapato ya biashara hizi ndogo.
Mfanyakazi katika biashara yako ndogo ya duka la rejareja
kama ndiyo kwanza unaanza wakati mwingine hana tofauti sana na mchimbaji au
mfanyabiashara asiyemwaminifu wa madini ya Tanzanite pale Mererani kwa
Serikali. Mfanyakazi au msaidizi wa duka asiyekuwa mwaminifu atafanya kila njia
ili akuibie senti zako kidogo ulizowekeza katika duka lako dogo bila kujali
kama umemuweka pale ili msaidiane, yeye apate kidogo na wewe pia upate kidogo.
Watu wana njia nyingi za kudhibiti na kusimamia biashara
zao hususani maduka haya madogomadogo ya rejareja wasiibiwe, lakini kuna hii
njia mpya niliyokuambia niliibuni, sijawahi kuisikia mahali pengine popote pale
niliianza mimi mwenyewe kama huu ukuta wa Mererani ulivyoanzishwa juzi.
Kwangu ilifanya kazi na nadhani kwa mtu mwingine inaweza
pia ikafanya kazi pia. Nimeamua kuiita mbinu hiyo jina, “TWO IN ONE STORE
MANAGEMENT SYSTEM” ni mfumo unaomwezesha mmiliki wa duka dogo la rejareja la
mtaji kuanzia milioni 3 kushuka chini kuweza kudhibiti mapato yake na faida
pasipo msaidizi au mfanyakazi kumuibia kirahisi. Mfumo huo unafanyakazi huku
mmiliki akiwa anafanya shughuli zake nyingine bila wasiwasi wowote.
Kumbuka kinachoyaua maduka mengi madogo ni usimamizi
mbovu unaopelekea wasaidizi ama wafanyakazi kudokoa mtaji na hatimaye duka kufa
kabla halijavuka mtaji wa shilingi milioni 3. Sasa ‘DAWA’ huu(MFUMO) utakwenda
kukusaidia kuondokana na stress zitokanazo na msaidizi asiyekuwa mwamnifu na
kukuacha wewe ukielekeza nguvu katika shughuli zako bila kuhofia tena kama
atakuibia na kuja kila siku asubuhi na jioni kukagua hesabu, mfumo utakupa muda
wa kutosha hata wiki nzima ndipo uje kukagua hesabu zako na pia unakupa urahisi
wa kubaini mapungufu yeyote yaliyotokea mara moja.
Mfumo huu unaweza kuupata kwa njia mbili, njia ya kwanza
ni kwa kuununua wenyewe moja kwa moja kwa bei ya shilingi elfu 5 ambapo unapata
pia na ofa ya kitabu cha MAFANIKIO YA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA bure kabisa.
Njia ya pili ni kwa kujiunga na Semina na masomo ya
Michanganuo na mzunguko wa fedha ndani ya Group la MICHANGANUO ONLINE kwa
shilingi elfu 10 ambapo unapata na ofa ya vitu vingine mbalimbali vipatavyo 10
vikiwemo vitabu vya Michanganuo ya biashara katika lugha ya Kiswahili na
kiingereza pamoja na masomo yote yaliyokwishapita na semina katika group hilo.
Group hili si lazima uwe unatumia wasap, hata ukiwa na email tu inatosha.
..................................................................
Kujiunga na group la MICHANGANUO ONLINE tuma namba yako ya watsap kwenye, 0765553030 au anuani yako ya Email pamoja na kiingilio sh. elfu 10 kupitia namba za simu 0712202244 au 0765553030 jina ni Peter Augustino Tarimo.
Kupata Vitabu BORA KABISA kutoka Self help Books Tanzania, tazama hapa chini au pia unaweza ukafungua hapa katika ukurasa huu wa vitabu wa; SMART BOOKS TANZANIA kujionea vitabu zaidi.
0 Response to "UKUTA WA RAIS MAGUFULI MERERANI MJASIRIAMALI UMEJIFUNZA KITU GANI HAPO?"
Post a Comment