KANUNI YA KUPATA FEDHA INAJULIKANA, UGUMU UPO WAPI? | JIFUNZE UJASIRIAMALI

KANUNI YA KUPATA FEDHA INAJULIKANA, UGUMU UPO WAPI?


Wajasiriamali Wengi na wale wote wanaotamani siku moja kuja kuwa wawekezaji wakubwa wangependa sana kupata njia ambayo wangeweza kuifuata hatua kwa hatua mpaka kuwafikisha kwenye mafanikio wanayoyatamani iwe ni maisha mazuri, utajiri au hata uhuru kamili wa kifedha.


Lakini pamoja na njia kujulikana wazi kabisa na kuwepo mifano ya matajiri au watu waliofanikiwa kupitia njia hizo, bado imekuwa vigumu wengi wetu kuweza kukamilisha mchakato huo. Wajasiriamali wengi hukatishwa tamaa  na kujikuta katika hali ambayo unaweza ukaifananisha na mtu aliye kwenye handaki(njia ndefu ipitayo chinichini kwenye ardhi mfano wa daraja refu). Shimo lenye giza nene na nuru hafifu sana huku kukiwa hakuna hatua zozote za maana zinazopigwa kusonga mbele na wakati mwingine bila ya kupiga hatua kabisa.


Kama wewe mjasiriamali ndio upo ndani ya handaki hili lenye giza nene na mishumaa michache sana inayokuwezesha kuona angalao  kidogo kwa kupapasa, utachukua hatua gani?


Mpenzi msomaji, somo hili lililo na funzo kubwa kwa mjasiriamali yeyote yule anaye ‘struggle’ hangaika litafundishwa leo hii katika Group la Whatsapp na Email la MICHANGANUO ONLINE. Tutaweza kufahamu kwa kina ni kwanini njia za kufanikiwa zinajulikana wazi lakini bado wengi wetu tunashindwa kufikia mafanikio ya kweli kimaisha. Sambamba na somo hili la leo pia kutakuwa na mfululizo wa tafsiri ya kitabu cha THINK & GROW RICH kwa Kiswahili na leo tunaanza rasmi Sura ya 10 baada ya jana kumalizia sura ya 9.

Masomo sasa ni kila siku kuhusu PESA, MICHANGANUO YA BIASHARA pamoja na TAFSIRI ya THINK & GROW RICH. Mtu anapojiunga pia tunamtumia papo hapo offa ya vitu(items) nyingine 10 yakiwemo masomo na mijadala yote iliyopita kwenye Group. Ikiwa hutumii Whatsapp masomo utapata kama kawaida kupitia Email au blogu ya private ya wanachama.

Ili kujiunga na masomo haya unaweza kulipia moja kwa moja kupitia namba zeti za simu, 0712202244  au 0765553030 jina hutokea Peter Augustino Tarimo, kisha tutumie ujumbe. Unaweza pia kuwasiliana na sisi kwa maelezo zaidi kupitia namba hizo au WHATSAPP 0765553030

0 Response to "KANUNI YA KUPATA FEDHA INAJULIKANA, UGUMU UPO WAPI?"

Post a Comment