Siyo rahisi uanzishe biashara mahali pakosekane biashara
nyingine au hata biashara zinazouza bidhaa sawa na za kwako katika eneo hilo.
Ingawa hauwezi ukawazuia kuuza kile
wakitakacho wao, lakini hapa kuna mbinu
ambazo ukizitumia, utakuwa kileleni juu zaidi kuliko wao. Ni mbinu 3
rahisi zilizothibitishwa za kuwapiku washindani wako kibiashara katika biashara
yeyote ile unayoifanya.
1. Punguza gharama.
Katika
jedwali lako la mapato na matumizi hakikisha unaorodhesha gharama zote
unazotumia, jiulize ni gharama ipi kati ya hizo unayoweza ukaipunguza lakini
angalia zipo gharama nyingine ambazo
hauwezi kamwe kuzipunguza kwani zitaleta athari mbaya zaidi katika biashara
yako kwa ujumla.
Kwa
mfano gharama kama mshahara wa mfanyakazi,
manunuzi ya bidhaa za kuuza ikiwa ni biashara inayohusisha bidhaa, na
gharama za matangazo au masoko kwa ujumla wake siyo vitu vya kupunguza hata
kidogo.
2 .Kuwa mbunifu
Biashara
yeyote ile, inahiaji mtu kuwa mbunifu katika mambo mbalimbali katika kuwafikia
wateja wako walengwa. Baada ya kufanya tathmini ya soko lako na kugundua siri
yako ya ushindi, fahamu ni mbinu gani za kipee utakazozitumia kuwavutia wateja
tofauti na wanavyofanya washindani wako. Unaweza hata ukabaini eneo ambalo
utaweka biashara yako lisilokuwa na ushindani mkubwa mathalani maeneo kama miji
mipya nk.
3. Toa huduma kwa wateja zinazopita
matarajio yao.
Kwa kuwapa wateja wako huduma nzuri za kipekee na
kuwajali utakuwa juu kushinda washindani wako
kwani watarudi tena na tena huku wakigeuka kuwa mabalozi wako wazuri kwa
wateja wengine wapya. Wateja hupenda kununua mahali ambapo hujiskia vizuri, na
kumuona mmiliki/muuzaji kuwa ni mtu anayejali maslahi na mahitaji yao kutoka
moyoni.
..............................................................
Ndugu msomaji wa makala hii, ile semina yetu kwa mwaka huu ya biashara na mbinu mbalimbali za kuongeza mtiririko wa fedha katika biashara zetu, inaendelea katika group letu la Whatsapp, email na blogu ya private ya darasa la michanganuo. Leo sikutoa taarifa mapema shauri ya kukatika kwa umeme lakini somo lipo palepale saa 3 usiku na leo nitafundisha, mada isemayo, KATI YA VITU HIVI 3, USIMAMIZI, MASOKO, NA UZALISHAJI NI KIPI MUHIMU ZAIDI KATIKA KULETA MAFANIKIO YA BIASHARA?
Chonde chonde mtu wangu usipange kukosa! pamoja na makala za nguvu kutoka kwa wadau wengine kwenye group kama vile wataalamu wa kuku kina FRANK MAPUNDA na wengineo.
UKITAKA VITABU PIA TEMBELEA, SMART BOOKS TANZANIA

0 Response to "NJIA 3 ZA UHAKIKA NA ZILIZOTHIBITISHWA ZA KUWAPIKU WASHINDANI WAKO KIBIASHARA"
Post a Comment