Watu wote Duniani waliowahi kufanya tafiti
mbalimbali kuhusiana na suala la mafanikio ya watu, katika majibu yao yote
inashangaza sana kukuta kwamba majibu hayo yanaweza yakafupishwa katika
muhtasari wa sentensi moja tu, tena yenye maneno machache sana tutakayokwenda
kuitazama katika makala hii ya leo. Sentensi hiyo ni hii hapa chini;
JIFUNZE KUTOKA KWA WALE WALIO NA UZOEFU.
Sentensi hii unaweza ukaamua kuitamka kwa
kutumia maneno tofauti lakini bado ikaendelea kubakia na maana ileile, unaweza
ukasema hivi; JIFUNZE KUTOKA KWA WALIOFANIKIWA, JIFUNZE KUTOKA KWA
WALIOKUTANGULIA, JIFUNZE KUTOKANA NA MAKOSA YA WENGINE, JIFUNZE KUTOKA KWA
MABINGWA. nk.
Utajifunza vipi kutoka kwa wale walio na
uzoefu?
Ni swali watu wengi sana hujiuliza, kwa mfano
hata wapo watu wengine huwa hawataki kabisa kusikia simulizi za mafanikio ya
watu mashuhuri, wakiamini kwamba ili waweze kujifunza namna walivyofanikiwa watu
hao ni lazima kwanza wakutane nao wenyewe ana kwa ana na hata ikiwa ni kitabu
kinachowahusu basi pia ni lazima kitabu hicho awe amekiandika mwenyewe mtu huyo
aliyefanikiwa. Lakini unaweza ukajiuliza, ni watu wangapi waliofanikiwa
huandika vitabu juu ya maisha yao wenyewe na njia walizopitia kufanikiwa
kimaisha? Jibu ni kwamba, ni wachache sana. Kwa hiyo penda tusipende ni lazima
tu tusome vitabu, majarida au taarifa zinazowahusu watu hao ikiwa tutataka
kujifunza mambo yao jinsi walivyofanikiwa, bila kujali kama taarifa hizo wameandika
wao wenyewe au la.
SOMA: Ni kitabu gani hautakisahau maishani?
SOMA: Ni kitabu gani hautakisahau maishani?
Kazi ya waandishi wa habari, waandishi wa
vitabu au hata waandishi wa kwenye mitandao ya kijamii ni kuandika na kutafiti
na wala siyo kile wanachokiandika basi ukute kinawahusu wao moja kwa moja . Mtu
mwingine anaweza kuona umeandika kuhusiana na mafanikio, yeye moja kwa moja
anakimbilia kuuliza, “ ‘Mwandishi hebu tueleze wewe umefanikiwa kiasi gani?’ au
‘nataka kujua mafanikio yako yakoje’
Si vibaya kuyajua lakini yafaa mtu kama huyo
akumbuke kwamba kazi kubwa zaidi ya wandishi au watafiti ni ile kazi ya
uandishi au utafiti wanaoufanya na mafanikio yao ni kuandika au kufanya utafiti mzuri wenye
faida kwa yule atakayeusoma au kuutumia. Nikiandika jambo likikusaidia basi
ujue huko ndiko kufanikiwa kwangu. Kwa hiyo bila kuwepo kwa watafiti na
waandishi ingelikuwa vigumu sana watu kujifunza kutoka kwa watu waliofanikiwa.
Tunajifunza kupitia kazi zao, ungewezaje kuzijua habari za kina Bill Gates,
Mzee Mengi, Mo, Mark Zuckerberg na
wengineo, wakati hata kuonana nao ana kwa ana hujawahi?
SOMA: Kijana wa umri mdogo anaweza kuanzisha biashara na ikafanikiwa?
SOMA: Kijana wa umri mdogo anaweza kuanzisha biashara na ikafanikiwa?
Kwanini inapendekezwa watu kujifunza kutoka
kwa walio na uzoefu?
Nilitoka kwenye mada kidogo lakini hebu
turudi tena. Sababu kubwa kwanini ujifunze kutoka kwa wale walio na uzoefu kama
ule unaotamani na wewe kuwa nao, kanuni kuu kuliko kanuni zote za mafanikio
nitazieleza katika mfano huu; Kwa mfano watu wote waliofanikiwa wana tabia
zinazofanana, hata ikiwa siyo kwa asilimia mia moja lakini angalao zinafanana. Na
hivyohivyo ndivyo ilivyokuwa kwa watu walioshindwa pia nao huwa wana tabia fulani
zinazofanana. Kupitia maandishi mbalimbali, hotuba zao, historia zao, na
taarifa zote kuwahusu imegundulika tabia za watu waliofanikiwa kuwa ni hizi
zifuatazo;
1. Walitumia
muda wao kwa uangalifu mkubwa sana na kuweza kukamilisha mambo mengi ndani ya
muda mfupi ukilinganisha na watu wengine wa kawaida.
2. Hutenda
kwa ufamisi mkubwa kazi zao, kwa usahihi na katika njia ifaayo huku muda wote
wakitafuta njia za kuboresha kile
wanachokifanya kwa ajili ya kupata matokeo bora zaidi. Kutokana na ubora huo wa
kazi na matokeo mazuri watu hawa hulipwa mishahara mizuri au kupata faida
nyingi kutokana na biashara zao.
Hata wewe na mimi tunaweza kutumia njia za
wale waliofanikiwa kuboresha maisha yetu kwa kupitia kanuni hii ya kujifunza
kutoka kwa wale waliofanikiwa au wenye uzoefu kutuzidi katika zile fani
tunazotamani na sisi kuja kufanya vizuri siku moja. Ili kurahisisha kazi hii,
ukiona huwezi kuonana moja kwa moja na mtu mwenye uzoefu na fani husika, basi
tafua machapisho kama vile vitabu nk. kuhusiana na mtu huyo au fani unayotamani
kufanya vizuri.
SOMA: Siri za matajiri na waliofanikiwa maishani.
SOMA: Siri za matajiri na waliofanikiwa maishani.
Nitatoa mfano hapa, tuseme labda wewe
unatamani kufanikiwa katika biashara ya ufugaji wa kuku, wanaweza kuwa ni wa
nyama, kuku wa mayai, kuku chotara au hata kuku wa kienyeji, mtafute mtu
anayefanya biashara hiyo moja kwa moja ujenge naye ukaribu, au ikishindikana
basi, jitahidi upate machapisho mbalimbali yanayohusu biashara ya ufugaji wa
kuku wa aina zote, michanganuo ya ufugaji wa kuku wa aina mbalimbali na hata vitabu vyenye habari za kuku
vilivyoandikwa na watu tofauti tofauti.
Kwa njia hiyo utafahamu kila kitu
walichofanya wale waliowahi kufuga kuku na wewe bila ya kupoteza muda mwingi
ukifanya “trial and error” au ukijaribu
kufahamu ni kipi kinachofanya kazi na ni kipi kisichofanya kazi, utajikuta
umepitia njia fupi ya mkato kabisa katika kuyafikia mafanikio kwenye ufugaji wa
kuku iwe ni wa mayai, nyama, wa kienyeji au hata kwa ajili ya kutotolesha
vifaranga.
Hatua inayofuata, amua sasa ni ufugaji wa
kuku wa aina gani unaotaka kufanya, kuku wa nyama, kuku wa kienyeji, au kuku wa
mayai? Baada ya hapo tekeleza mpango wako sasa ukiwa na taarifa zote muhimu
kuanzia mchanganuo wote wa gharama na faida ya mradi mzima.
……………………………………………………
Ndugu msomaji wa makala hii,
nimekuandalia kifurushi cha michanganuo kamili mitatu ya biashara za ufugaji wa
kuku, kuku wa nyama, kuku wa kienyeji wa mayai na kuku wa kisasa wa mayai
kiitwacho(MKOMBOZI CHICKS PLAN 3PACKS).
Michanganuo hii ni kamili(full) ina kila kitu kuanzia wazo lenyewe la ufugaji,
utekelezaji wote, mpaka mchanganuo wote wa hesabu za gharama mbalimbali na mapato
yanayotokana na biashara hii.
Michanganuo hii inajibu maswali
mengi wafugaji wapya wa kuku na hata wale wazoefu wanayojiuliza mara kwa mara
kama vile, nahitaji kiasi gani cha mtaji kuanza kufuga kuku 100, 200, 500 nk.,
gharama zote za mradi ni kiasi gani tangu kuanza mpaka mwisho, ni mbinu gani za
kutumia ili kupunguza gharama za ufugaji wa kuku, ni vyakula gani vinavyotakiwa
kulisha kuku wa aina mbalimbali? Kati ya kuku wa kisasa na wa kienyeji, ni yupi
aliye na faida zaidi, kati ya kuku wa nyama na wa mayai ni yupi anayelipa zaidi
nk.
Bei ya kifurushi hiki ni
shilingi elfu 10, na ukishalipa unapata na offa ya kuingia katika GROUP la
WHATSAPP la MICHANGANUO ONLINE ambalo ndani yake kunapatikana watu wenye uzoefu
wa biashara mbalimbali ikiwemo ufugaji wa kuku wa aina zote. Unapewa pia na
offa ya vitabu na vitu vingine mbalimbali yakiwemo masomo yote yaliyopita. Ofa
hizi ni za muda maalumu tu, muda ukiisha kila kitu kitaendelea kuuzwa peke yake
kama kilivyo, hivyo wahi usije kuchelewa. Ikiwa hutumii whatsapp hamna shida
kwani tunatumia njia 3, email pamoja na Blog ya private.
SIMU: 0712202244
AU 0765553030
WHATSAPP: 0765553030
JINA: Peter Augustino Tarimo
Kwa vitabu vya biashara,
ujasiriamali na maendeleo binafsi tembelea SMART BOOKS TANZANIA.
0 Response to "KANUNI KUU YA MAFANIKIO DUNIANI ILIYO KUBWA KUSHINDA ZOTE"
Post a Comment