UNAPOANZISHA BIASHARA YAKO, VITU HIVI (3) USITEGEMEE KUFUNZWA NA MTU YEYOTE | JIFUNZE UJASIRIAMALI

UNAPOANZISHA BIASHARA YAKO, VITU HIVI (3) USITEGEMEE KUFUNZWA NA MTU YEYOTE

KUANZAISHA BIASHARA
Unapochukua uamuzi wa kuanzisha biashara yako mpya, kumbuka ya kwamba vipo vitu ambavyo ni wewe mwenyewe unayetakiwa kuvigundua wakati ukiwa katika mchakato wa kuiendesha biashara yako, hakuna mtu atakayeweza kukufundisha uvifanye na hata akitokea mtu akafanya hivyo wala hutamuelewa.


Yapo mambo mengi ya msingi unayojifunza kutokana na uzoefu unaoupata mbali na elimu au mafunzo rasmii ya biashara na ujasiriiamali unayoweza kuwa uliyapata mahali kwingine mfano kama hapa katika blogu hii unayosoma sasa. Na yale unayojifunza kutokana na uzoefu au vitendo halisi ndiyo pengine yaliyokuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kukuwezesha kuiendesha biashara yako kwa mafanikio makubwa zaidi. Miongoni mwa vitu hivyo nimeviorodhesha hapa  chini;


1. Kamwe usije ukabweteka. 
Kujisahau kunawafanya wafanyabiashara wengi  hatimaye kuanguka hata ikiwa walishaanza kupata mafanikio. Mara nyingi watu hawategemei kama jambo dogo kama hili ni somo kubwa wanalopaswa kujifunza mpaka bada yameshawafika ndipo huja kugundua kumbe ni kitu muhimu.

Kumbuka hakuna  mikakati  inayoweza kudumu milele, soko unaloliona leo au ulilolliona jana silo litakalokuwepo kesho, linaweza likaanguka muda wowote, halikadhalika na bidhaa au huduma unazooweza kuona leo hii zinafanya vizuri sokoni, muda wowote zaweza kudorora, hivyo mipango na mikakati yako ni lazima ifanyiwe uhakiki kila baada ya muda na ndiyo maana katika mafunzo ya jinsi ya kuandaa mpango wa biashara yanayopatikana ndani ya kitabu  cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI, umuhimu wa kufanya ulinganisho baina ya mpango wa biashara yako na hali halisi umesisitizwa sana. Ni sharti kila baada ya muda fulani ucheki kujua ni kipi kimeenda kama ulivyopanga na ni kipi hakikwenda ili uweze kujua ufanye nini zaidi au upunguze nini.


2. Huwezi ukafanikiwa peke yako.
Kufanya biashara kama mtu binafsi haimaanishi kwamba upo peke yako, Unaweza ukajidai kwamba mafanikio yako yametokana na nguvu zako binafsi lakini kumbuka uungwaji mkono mkubwa ulioupata kutoka kwa watu mbalimbali ikiwemo familia yako, mke, watoto, ndugu jamaa na marafiki, wajomba, shangazi, mama na baba wadogo, mashemeji nk. Hata kitendo tu cha kukutakia mema na kukuombea ufanikiwe, kisaikolojia ni msaada mkubwa kwako katika kufanikiwa biashara yako. Usaidizi hauishii tu kwa watu bali hata vitabu, DVD na mafunzo mbalimbali unayoyapata pia huhesabika kama usaidizi.

3.Mshindani wako mkubwa ni wewe mwenyewe.
Kila siku unajitahidi kuwa bora kushinda siku iliyopita, hii  ni kusema kwamba wewe wa leo unashindana na wewe wa jana na, mara zote ungependa umshinde wewe yule wa jana.


Kuna mambo mengi unayoweza kujifunza kutokana na uzoefu wako binafsi katika biashara, mengi ya hayo huwezi ukaelewa mantiki yake mpaka umeingia front (msari wa mbele) mwenyewe kwenye biashara. Kama wewe ni start up, ndiyo unaanza au unapanga kuanza siku moja basi usisubiri kujua kila kitu kuhusiana na ABC za biashara na ujasiriamali, wewe anza tu,mengine utajifunza mbele ya safari kutokana na uzoefu.
……………………………………………………………………....

Kujifunza zaidi, usikose vitabu vyako vifuatavyo kutoka Self Help Books Tanzania,

Masiliano yetu ni 
0712202244  au  0765553030, 


HARDCOPY SH.30,000/=

SOFTCOPY SH.10,000/=


HARDCOPY SH.15,000/=

SOFTCOPY SH. 5,000/=


HARDCOPY SH.7,000/=

SOFTCOPY SH.3,000/=

Tupo Mbezi karibu na  stendi kuu ya mabasi. 

Kwa vitabu zaidi na maelezo tembelea ukurasa; SMART BOOKS TANZANIA

0 Response to "UNAPOANZISHA BIASHARA YAKO, VITU HIVI (3) USITEGEMEE KUFUNZWA NA MTU YEYOTE"

Post a Comment