IPO SIKU YANGU TU WA GOODLUCK GOZBERT NI MOJA YA NGOMA NIPENDAZO MIMI | JIFUNZE UJASIRIAMALI

IPO SIKU YANGU TU WA GOODLUCK GOZBERT NI MOJA YA NGOMA NIPENDAZO MIMI

IPO SIKU YANGU, NGOMA NIPENDAZO




Muziki ni moja ya vitu duniani ambavyo haviegemei upande wowote ule kwa kimombo huitwa ‘universal’. Kinachonifanya niseme hivyo ni sababu kwamba wewe unayesoma hapa unaweza ukajiuliza swali, “Hivi Peter na blogu yake hii sasa ameanza kuchoka kuandika na ujasiriamali na elimu ya biashara na badala yake anataka kuhamia kwenye muziki wa injili au gospel?

SOMA: Wimbo mpya wa Jose Chameleon, Tubonge, naupenda sana

Lakini nirudie tena kusema muziki kama ulivyowahi kuwa na ambavyo utabakia kuwa siku zote ni lugha ya kiulimwengu ambayo haina ubaguzi wa aina yeyote ile, na ndiyo maana unaeza kukuta mtu hajui kinaijeria kabisa au kihispaniola lakini utakapokuta akisikiliza muziki kutoka maeneo hayo ya dunia kwa hisia kali utadhani labda kuna siku moja alishawahi kufika na kujifunza lugha hizo. Haki ni hiyo hiyo hata katika maeneo mengine kwa mfano, jinsia, dini, rangi, kabila, madhehebu na hata umri.

SOMA: Nina wa Nyiboma na Pepekalee,  nikiukumbuka napata wazimu!

Ndiyo maana utakuta kwa mfano mwanamuziki kutoka Marekani anaweza akaingia kirahisi tu Korea ya kaskazini kenda kutumbuiza licha ya uadui mkubwa uliopo baina ya mataifa hayo. Si hivyo tu hata enzi za vita baridi kati ya iliyokuwa Usoviet na Marekani, Michael Jackson aliingia Moscow kirahisi kabisa na kupagawisha mashabiki lukuki waliosahau kabisa tofauti zao za kiitikadi wakati huo.

Leo hii rasmi nimeanzisha kipengele hiki ambacho kitakuwa kikinihusu mimi binafsi zaidi nikielezea hisia zangu kimuziki, nadhani kila mtu anapenda muziki wa aina yake, muziki ninaoupenda mimi siyo lazima na mtu mwingine aupende lakini pia kutoa hisia zako binafsi siyo vibaya. 

SOMA: Muziki ulipokuwa muziki, Katitu boys band na miziki mingine ya Kikamba na Kikuyu, je unakumbuka wapi na lini?

Binafsi kama nilivyotangulia kusema sina mapenzi na mziki wa aina moja tu, napenda miziki mchanganyiko ndiyo maana kama utanifuatilia kwani kipengele hiki siyo lazima kama wewe ni shabiki wa blogu hii ukisome unaweza kuachana nacho na kupita, utaona mara kwa mara kila hisia zangu zitakaponirudisha kwenye muziki fulani nitaandika na kuweka audio hapa au video kama njia ya kujirefresh mwenyewe wakati ninapokuwa nimechoka kwa mfano wazo la nyimbo hii ya Ipo siku wa Goodluck Gozbert limeibuka akilini mwangu usiku wa saa 7 wakati nimechoka kuandika.

SOMA: Professa J: Historia ya muziki wa Bongo fleva, sisi ni wachonga barabara(tingatinga)


Mbali na midundo ya vyombo katika wimbo huu kunisuuza pia ujumbe wake uliopo kwenye maneno unanigusa na kuniingia moyoni hasa ninaposikiliza vipande vya mashairi haya, yamegusa karibu kila sekta muhimu za maisha ya leo, umasikini, magojwa, ndoa, biashara, uvumilivu, kudharauliana, waganga wa kienyeji, kumcha Mwenyezi Mungu na hata mambo ya michepuko siyo dili nayo yapo. Una ujumbe wa kutia moyo(Inspirational) kwamba bila kujali ni vikwazo vya aina gani unavyopambana navyo, unapaswa kusonga mbele na ipo siku tu utafanikiwa.

SOMA: Milliano lyrics, Dr. Josee Chameleone: Sikiliza mashairi ya wimbo na video yake.


Haya hapa mashairi ya wimbo, Ipo siku yangu tu wa Goodluck Gozbert

Ni mbali Nimetoka,
Tena ni ajabu kuwa hai maana
Ningeshakufaaga

Ni mengi nimeona
Tena ya kuvunja moyo
Labda ningeshakuacha Mungu

Kama ni misongo ya mawazo
Magojwa ma nimepitia, nimezoea

Maumivu ya kudharauliwa
umasikini kila siku
Ninajipa mooyo

Ipo siku yangu tu
Ipo si siku
Ipo siku yangu tu, nami niba niba nibarikiwe x2

Nami nibarikiwe
Nibarikiwe
Aah nibarikiwe
Nibarikiwe
Nami nibarikiwe
Nibarikiwe
niba niba nibarikiwe x2

Aah Ooh nimeona
mmh
Aiyaya aiyaya aiyaya
Mmh

Ingawa kwa sasa wananisema vibaya
Nami sishangai najua ni ya wanadamu hayoo
Ingawa sipati na ni kwa muda mrefu
Siachi kuoomba  Mungu si kiziwi
Binadamu wema ukiwa nacho ooh
Kwa sasa waniepuka sina rafiki wa dhati

Kama ni misongo ya mawazo
Magonjwa ma nimepitia
Nitazoea
Maumivu ya kudharauliwa
umasikini kila siku ninajipa moyo

Ipo siku yangu tu
Ipo si siku
Ipo siku yangu tu nami
Niba niba nibarikiwe x2

Nami nibarikiwe
Nibarikiwe
aah nibarikiwe
Nibarikiwe
Nami nibarikiwe 
Nibarikiwe
niba niba nibarikiwe x2

Miaka imepita
unaombaga mtoto hupati
Vuta subira maana yeye hachelewi
Ona biashara imeandamwa mikosi
hupati usimwache Mungu
Waganga watakuponza
Mpo kwa ndoa ila imani amani huna
Msimwache Mungu mchepuko siyo jibu

Umeugua tumaini la kupona hakuna
usimtazame mwanadamu
siku yako imekaribia
hey

najua ayaya najua ayaya


Je, ungependa kudownload mashairi ya wimbo huu wa Goodluck Gozbert kwa ajili ya kuprint au kuhifadhi usome baadae?



.........................................................................................................................

Maelezo zaidi kuhusiana na vitabu hivi na vinginevyo, tembelea ukurasa wa SMARTBOOKS TANZANIA, vitabu muashara kwenye smart phone yako.

0 Response to "IPO SIKU YANGU TU WA GOODLUCK GOZBERT NI MOJA YA NGOMA NIPENDAZO MIMI"

Post a Comment