KUSIMAMIA BIASHARA YAKO NDOGO UNAONA NI KAZI NGUMU? BORA UIACHE, UTAVUNA MABUA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

KUSIMAMIA BIASHARA YAKO NDOGO UNAONA NI KAZI NGUMU? BORA UIACHE, UTAVUNA MABUA

udhibiti na usimamiaji wa biashara ndogondogo
Usimamizi wa biashara nyingi umekuwa ni changamoto na sababu kubwa inayochangia kuanguka kwa asilimia kubwa ya biashara hizo hata kabla ya mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake. Kusimamia vizuri biashara kunajumuisha mambo mengi yakiwemo, udhibiti wa mapato yanayotokana na mauzo ya bidhaa au huduma kwenye biashara, udhibiti  wa mali na rasilimali za biashara ukiwemo muda pamoja na udhibiti wa manunuzi na bajeti.


Waanzilishi wengi wa biashara hujikuta katika mtihani mgumu hasa pale wanapofikiri kwamba wakishakuwa mabosi basi kila kitu wanawaachia wasaidizi au wafanyakazi kwenye biashara zao kuanzia meneja mpaka mtunza stoo, kumbe siyo hivyo inabidi uhakikishe unafanya usimamizi wa karibu kabisa na hata ikiwezekana wewe jukumu la umeneja ujivike mwenyewe kusudi biashara yako iweze kuvuka kirahisi katika ngazi hii ngumu ya kuanza kwa biashara.


Unapofanya kosa la kuajiri wafanyakazi na kuwaachia kila kitu wasimamie wao wenyewe, maana yake umewaambia wajitafutie na wao mitaji yao kusudi wakafungue biashara zao. Kumbuka hakuna mtu anayependa kuajiriwa, kila mtu angependa kuanzisha na kusimamia biashara yake mwenyewe kikamilifu hata ikiwa ndogo ili aweze kupata faida kubwa na nono zaidi, sasa anapokuja kwako kuomba ajira ujue siyo mjinga, kama angekuwa na mtaji pengine hata wewe ungeweza kuwa mfanyakazi wake. Ndiyo maana kukawekwa mifumo mbalimbali ya usimamizi wa biashara au miradi kuzuia wanaofanya kazi katika miradi au biashara hizo wasije wakazihujumu kwa namna yeyoe ile.

Kwa bahati mbaya katika biashara ndogo ndogo, udhibiti ni suala tete kidogo kutokana na udogo wa mtaji. Mfanyakazi akidokoa pesa kidogo tu, athari yake ni kubwa ajabu!. Kwa mfano unaweza kuajiri kijana wa kukaa dukani kwako au biashara nyingine yeyote ile, yaweza hata ikawa ni saluni au mgahawa, au hata mradi wa kuku wa mayai,  usipojitahidi kufanya stoku mara kwa mara au kuhesabu mali za dukani kwako, kijana huyo anaweza akawa kila siku anajiwekea kiasi fulani cha fedha na pindi lengo lake litakapotimia, humuoni tena.


Atasingizia vitu kibao, mara “oo.. mimi naumwa…nataka kupumzika…nimefiwa kijijini” nk. Ilimradi tu aache kazi na siku mbili tatu unamkuta keshafungua biashara yake. Sasa kwa kuwa huna ushahidi wala kumbukumbu nzuri za mahesabu ya duka lako(biashara yako), basi na wewe unaishia kumuacha tu aende zake hivi hivi. Lakini kama siku ya kwanza unamuajiri mlipigiana mahesabu, mkaorodhesha kila kitu kwenye daftari, ukamwambia “nakukabidhi kiasi hiki cha mtaji” na kila siku manunuzi ya vitu ukarekodi mahali ili kuja kubaini faida itakayopatikana dukani kila siku mpaka siku ya mwisho mtakapokuja kufanya stock nyingine, basi kijana huyo itamuwia vigumu kwelikweli kudokoa.

Na isitoshe mnasaini mahali kwa masharti kwamba akiingiza hasara(shoti), basi atawajibika kulipa kwa fedha zake za mshahara. Hapo sasa wewe usiwe mzembe hakikisha mnafanya mahesabu kikamilifu na kwa wakati, siyo mara umefanya leo kesho umeacha. Ujue wafanyakazi ni wajanja sana, huwa wanawasoma matajiri zao kujua udhaifu wao upo wapi. Wengi wakishajua huwa hawafanyi ajizi.


Kwahiyo biashara ni USIMAMIZI asikudanganye mtu bwana, ndiyo maana katika kitabu cha MAFANIKIO YA BIASHARA.DUKA LA REJAREJA, mwandishi kwa kutumia uzoefu wake mkubwa katika biashara hiyo kwa muda wa miaka 12, ameweza kuainisha mifumo mbalimbali inayomuwezesha mmiliki wa duka hasa la rejareja au biashara nyingine yeyote ile ya rejareja kusimamia na kudhibiti hesabu za biashara yake kikamilifu, jambo linalomuwezesha kusimamia hata maduka zaidi ya sita kwa wakati mmoja bila ya kupoteza mapato yake ovyo.

Si hivyo tu katika kitabu hicho pia mbinu mbalimbali za uendeshaji wa biashara ya rejareja zimeelezwa kwa kina ikiwa ni pamoja na mchanganuo mzima wa biashara hiyo wenye kila kitu, makosa mbali mbali yanayoweza kukufanya uhisi umelogwa, jinsi ya kuzuia chuma ulete dukani au kwenye biashara yako, siri nzito wenye maduka makubwa hawatakueleza hata uwape pesa nk.

Mbinu hizo zimezingatia makundi mbalimbali ya jamii na makundi ya wakongwe wa biashara hizi za rejareja kuanzia Wahindi, Wachagga, Wapemba, Wakinga na hata jamii moja ya kabila linalopatikana huko China balaa kwa biashara hizi, hujifanya wajingawajinga kumbe ni moto wa kuotea mbali, anapokuuzia kitu utanunua tu hata akuambie bei kubwa vipi, wana tekiniki balaa!.


Kwa hiyo ndugu msomaji wa makala hii, nakusihi kama wewe ni mmiliki wa biashara ndogo, una lengo la kuanzisha biashara ndogondogo au hata una mpango wa kumuajiri mtu kazi ya kukaa kwenye biashara yako ndogo,  hakikisha suala la usimamizi unalipa kipaumbele cha kwanza, lifanye kuwa ndiyo sirikuu ya mafanikio ya biashara yako.

Ni bora hata mfanyakazi mwenye tabia ya kukimbiza wateja kwa kauli zake mbovu, unaweza ukamrekebiasha, lakini ndugu yangu, huyu aliye na tabia ya kuhamisha mtaji wako utarekebisha tatizo hilo saa ngapi wakati ukijakuchukua hatua yeye keshafungua biashara yake? So be carefull, usije vuna mabua bure.
………………………………………………………………………………..
Vitabu 3 vya Self Help Books Tanzania kikiwemo kile cha MAFANIKIO YA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA, unaweza ukavipata kwa urahisi na ukiwa mahali popote pale nje na ndani ya Tanzania kupitia E-mail yako kama PDF file au softcopy.

Cha kufanya tu ni kutuma pesa ya kitabu husika kwenye namba za simu 0712202244  au  0765553030 jina Peter Augustino Tarimo, pamoja na anuani yako ya E-mail kwa njia ya meseji, kisha na sisi tunakutumia kitabu/vitabu muda huohuo.
Hatujawahi kamwe kumsumbua au kumcheleweshea mteja anayetuma fedha yake kununua kitabu.


Vitabu vya karatasi(Hardcopy) pia vinapatikana  na kwa Dar es salaam tunakuletea mpaka pale ulipo au unafika Mbezi stendi kwa Msuguru tunakopatikana. Piga pia, 0712202244  au 0765553030 au sms kufahamu zaidi.


SOFTCOPY SH.  5,000/=
HARDCOPY SH. 10,000/=



SOFTCOPY SH. 10,000/=
HARDCOPY SH. 20,000/=


SOFTCOPY SH.  3,000/=
HARDCOPY SH.  5,000/=

0 Response to "KUSIMAMIA BIASHARA YAKO NDOGO UNAONA NI KAZI NGUMU? BORA UIACHE, UTAVUNA MABUA"

Post a Comment