JE WEWE NI KIONGOZI WA DINI, ASASI, SACCOS, AU KIKUNDI CHA KIJAMII? | JIFUNZE UJASIRIAMALI

JE WEWE NI KIONGOZI WA DINI, ASASI, SACCOS, AU KIKUNDI CHA KIJAMII?

Unajua katika shughuli zozote zile zinazohusiana na taarifa mfano wa makala kama hii unayoisoma hapa sasa hivi, suala la mrejesho “feedback” ni kitu muhimu sana na ndiyo kichocheo kikubwa kinachoweza kusababisha mchakato mzima wa shughuli yenyewe ya ubadilishanaji taarifa kuwa endelevu. Naandika haya, kwani sikutegemea kile nilichopata kama mrejesho kutoka kwa Mchungaji huyu kutoka Mtwara.  
Wawezeshaji wa elimu ya biashara na ujasiriamli
Wawezeshaji, viongozi wa dini na kijamii.
Leo hii majira ya mchana mteja mmoja wa kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI kama ilivyokuwa kawaida kwa wateja wengine wengi wanaonunua vitabu kutoka hapa Self Help Books Tanzania mara kwa mara, baada ya kufanya muamala na mimi kumtumia kitabu kupitia anuani yake ya email aliyonitumia, hatimaye usiku huu alinitumi ujumbe ufuatao,

“Ninashukuru sana kwa masomo mazuri yaliyokuwa ndani ya kitabu hiki, tangu mchana nimekuwa nikipitia baadhi ya sura za kitabu, kwa kweli ni kizuri. Kesho nafundisha watu hapa Mtwara kanisa la(sijataja kanisa lenyewe) katika semina ya ujasiriamali ambayo itahusisha Wachungaji na Wainjilisti. Kitabu hiki naamini kitakuwa msaada mkubwa sana kwangu.
Ubarikiwe sana na Bwana,
Mchungaji (Jina sijalitaja pia)”  

Kwa kweli wakati nauza kitabu hicho sikuwa na wazo kabisa kama mteja ninayemuuzia anaweza akawa ni mchungaji, kiongozi wa dini mpaka pale nilipoona mrejesho huo na yeye kujitambulisha kuwa ni mchungaji. Binafsi nilifarijika sana kuona hata viongozi wa dini, asasi ama vikundi mbalimbali vya kijamii wakitumia vitabu vyetu kwa aili ya kufundishia semina mbalimbali za ujasiriamali, biashara na maisha kwa ujumla kwani moja ya malengo yetu makuu ni kuona jamii na hasa wananchi wengi wa kawaida wakipata ujuzi wa kufanya biashara kusudi waweze kuboresha maisha yao zaidi.

SOMA: Gharama za kutuma vitabu vya 'Self Help Books' Mikoani ni shilingi ngapi?


Vitabu vyetu vyote vitatu, kile cha Michanganuo na Ujasiriamali, Mafanikio Biashara ya Duka La Rejareja, na hata Mifereji 7 ya Pesa, vyote ni vitabu ambavyo mkufunzi yeyote yule wa semina za ujasiriamali au mwezeshaji katika vikundi mbalimbali vya kijamii anaweza akavitumia katika kuandaa mada zake. Hatuzuii kufanya hivyo ikiwa mtu anafanya kwa lengo la kuelimisha jamii.






0 Response to "JE WEWE NI KIONGOZI WA DINI, ASASI, SACCOS, AU KIKUNDI CHA KIJAMII?"

Post a Comment